Matukioa katika picha Ibada ya Jumapili ya tarehe 17/09/2023, katika Usharika wa Źory nchini Poland, ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ambapo kutoka Bara la Afrika ni Mjumbe pekee kwenye Kamati ya Ibada na Muziki kwenye mkutano Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF) unaoendelea nchini Poland .Wajumbe wa Mkutano huo wamepata nafasi ya kushiriki Ibada ya Jumapili kwenye sharika mbalimbali. Ujumbe mkuu wa Mkutano huu ni kutoka kitabu cha Waefeso 4:4-6 "MWILI MMOJA, ROHO MMOJA, TUMAINI MOJA".