Tarehe 21/09/2023 akiwa nchini  Ujerumani Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alialikwa kwenye kiwanda cha kutengeneza makontena na stoo maalum zinazozuia moto, kiwanda hiki  kinasimamiwa na kampuni ya  DENIOS. Hapa Baba Askofu alikutana  na baadhi ya marafiki walioonyesha moyo wa kujitolea kufadhili mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Makose kilichoko kwenye Usharika wa Mwangoi. Kutoka kulia ni Bw. Ernst-Ludwig Homann (anayesimamia mawasiliano kati ya Usaharika wa Mwangoi na Usharika rafiki wa Bergkirchen - Ujerumani), Bw. Helmut Dennig (Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya DENIOS) na Askofu Dkt. Mbilu. Mradi huu ambao utatekelezwa na kusimamiwa na Usharika rafiki wa Bergkirchen ni miongoni mwa miradi kadhaa ya maji iliyowekwa kwenye eneo la Usharika wa Mwangoi wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Tarehe 23/09/2023 kilifanyika kikao cha NED ROUND TABLE kilifanyika Bethel Ujerumani.  Hapa Baba Askofu alikutana na  marafiki mbalimbali wa Dayosisi wenye urafiki na Majimbo na Sharika na Vituo vya Dayosisi. na kuwashirikisha juu ya deni la Dayosisi uongozi wa Baba Askofu Dkt. Mbilu walilorithi ambalo linasumbua Dayosisi na maendeleo ya Dayosisi kwa jumla. Wengi wameshukuru kupata maelezo sahihi ya madeni haya tofauti na taarifa mbalimbali za upotoshaji wanazosikia mitaani.

KATIKA PICHA: Katikati ni Mkuu wa Jimbo la Vlotho Dorothea Goudefroy ambaye alihudhuria kikao hiki cha NED ROUND TABLE

 

Baadhi ya watumishi mbalimbali waliowahi kufanya kazi Lutindi Mental Hospital zamani tulikutana nao. Walitamani kusikia maendeleo ya kituo cha Lutindi Mental Hospital na kipekee katika wakati huu ambao kituo kinakabiliwa na madeni ya Dayosisi.

Tarehe 24.09.2023 Baba Askofu Dkt. Mbilu aliongoza Ibada katika Usharika wa Apostle Gemeinde kwenye mji wa Bielefeld. Usharika huu unaratibu shughuli za mahusiano kati ya Usharika huu na Sharika za Lutindi, Bungu, Tamota, Manka, Mbangulu na Luthindi Mental Hospital kwa muda mrefu sasa.

Tarehe 25/09/2023 Baba Askofu Dkt. Mbilu, alitembelea Ofisi Kuu ya UEM iliyoko katika mji wa  Wuppertal na kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa UEM Mch. Volker Martin Dally (Kushoto) pamoja na Bw. Timo Pauler (Kulia) Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala ya UEM.