Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka Mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”
KATIKA PICHA: Ibada ya Mazishi ya Marehemu Mzee Raphael Yohana Shebila ilyofanyika katika Kijiji cha Shashui Mzungu Soni nyumbani kwa Marehemu na baadaye mwili wake ulipumzishwa katika eneo la makaburi ya familia leo tarehe 11/04/2024.
 
Marehemu Mzee Raphael Shebila alizaliwa tarehe 05/03/1942 katika kijiji cha Shashui Mzungu Soni na kuitwa Mbinguni tarehe 08/04/2024 akiwa na umri wa miaka 82. Marehemu Mzee Raphael ni Baba Mazazi wa Mtumishi wa Ofisi Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwinjilisti William Shebila.
Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, unaendelea kutoa pole kwa,familia ya Marehemu Mzee Raphael Yohana Shebila ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.