Leo tarehe 12/12/2020 yamefanyika Mahafali ya kumi na moja katika Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) ambapo Jumla ya wanafunzi 30 wamehitimu masomo yao kama ifuatavyo .Astashahada ya Tehama (Basic Technician Certificate in Computing, Information and Communication-Mhitimu 1.Shahada ya Awali ya Sayansi katika Afya ya Akili na Utengemao (BSc Mental Health and Rehabilitation) Wahitimu 24.Shahada ya Uzamili katika Elimu Maalumu (Master of Education in Special Education) Wahitimu 5.

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajjat Mwanasha Tumbo amesema kuwa serikali ipo bega kwa bega na uongozi wa chuo kikuu cha Sebastiani Kolowa Memorial University (SEKOMU) ili kuhakikisha Chuo kinarudi katika ufanisi wake kwakuwa ndio chuo pekee katika Mkoa wa Tanga ambacho ni fursa kwa mkoa mzima wa Tanga hivyo kuutaka uongozi wa Chuo kufanya kila linalowezekana ili kufanikisha jambo hilo.

Aidha amewataka wahitimu kutumia fursa zilizopo na kujitambua sambamba na kutumia fursa zilizopo ili kujiletea maendeleo na kupata mabadiliko chanya na asiyefanya hivyo ataona fursa zikimpita na kuachwa nyuma kimaendeleo.
Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo hicho Prof. Vincent Kihiyo ameishukuru serikali kwa kuendelea kuunga mkono vyuo binafsi hususani katika maswala ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu sambamba na kuwapongeza wahitimu licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali.


Mahafali hayo yalihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali akiwemo Askofu Mteule wa Dayosisi ya Kaskazini Masharika Dk Msafiri Joseph Mbilu,Msaidizi wake Mch Michael Kanju,Kaimu katibu Mkuu Mch. Godfrey Walalaze, huku viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Lushoto January Lugangika pamoja na wageni mbalimbali walihudhuria.