Print

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania . Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) yenye Makao Makuu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga ni miongoni mwa Dayosisi 28 za KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri za kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu wote. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi moja  ya MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (PROJECT COORDINATOR) kwa vijana wote  (Wakristo) 

NAFASI NA WAJIBU WA MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA (PROJECT COORDINATOR).

1.1 CHILD AND YOUTH DEVELOPMENT CENTER COORDINATOR (CYDC)- MRATIBU WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANA.

Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto na Kijana ni mwajiriwa wa Kanisa na atatumika  katika kituo cha maendeleo ya Mtoto na kijana (KKKT – SINDENI BWAWANI – TZ1212) kilichopo Sindeni – Wilaya ya Handeni. Katika utendaji wake wote wa majukumu /wajibu atawajibika kwa Mchungaji kiongozi na kusimamiwa na Kamati ya huduma ya Mtoto. Atasimamia utendaji wa watendakazi wengine katika kufanikisha shughuli za maendeleo ya ujumla ya Mtoto na kijana. Atasimamia maono ya maendeleo ya ujumla ya Mtoto na kijana na amali za huduma wakati wote wa Uhai wa kituo cha Huduma ya Mtoto.


Kazi muhimu na wajibu wa Mratibu wa Kituo Cha Maendeleo Ya Mtoto Na Kijana ni kama ifuatavyo:


1.2 SIFA ZA MRATIBU WA KITUO CHA MAENDELEO YA MTOTO NA KIJANAELIMU:

1.3 UJUZI/UFAHAMU/SIFA NYINGINE:


NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.

Maombi yote yatumwe kwa  

Katibu Mkuu KKKT-DKMs
S.L.P 10,
LUSHOTO TANGA
Kupitia email ya :  This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


1.Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, wasifu wa mwombaji (Cv), cheti cha kuzaliwa, na nakala za vyeti vyote vya ujuzi mbalimbali (kama unavyo).
2.Barua ya utambulisho kutoka kwa Mchungaji wa Kanisa unaloabudia kwa sasa (Lazima)
3.Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/03/2025
4.Waombaji watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye usaili (Interview)
5.Tarehe ya usaili watajulishwa kwa njia ya simu