Print

 

Leo tarehe 27/11/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Mshihwi kanda ya Magoma, Jimbo la Tambarare, ambapo vijana wapatao 63 walipata kipaimara. 

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu. Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi, Kwaya, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Mshihwi. 

Katika risala ya vijana hao waliopata kipaimara wamemshukuru Baba Askofu Dkt. Mbilu kwa kutenga muda wake na kushiriki katika Ibada hiyo, kipekee wameushukuru uongozi wa KKKT-DKMs pamoja na watenda kazi wengine wa KKKT-DKMs kwa namna wanavyo fanya kazi kubwa ya kuirejesha Dayosisi katika hadhi yake ya awali.

Katika siku hii vijana hao wanapothibitisha imani yao ya Kikristo waliyobatizwa nayo walipo kuwa watoto wadogo wameungana na uongozi wa Dayosisi katika kuunga mkono masuala ya elimu kwa kuchangia jumla ya Tsh.189,000.

Awali Baba Askofu aliyeambatana na msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Mch. Michael Mlondakweli Kanju walipata nafasi ya kufungua nyumba ya mtumishi katika Usharika huo wa Mshihwi kanda ya Magoma.