Print

Leo tarehe 28/11/2021 ni siku ya Bwana ya kwanza katika maajilio, advent ya kwanza.kila mwaka wanawake wanapata nafasi ya kuongoza Ibada na kufanya maombi na maombezi kwa ajili ya familia,Sharika,Majimbo na Dayosisi kwa ujumla.Sharika zote za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki zimeungana katika maombi hayo.

Katika Ibada  iliyoongozwa na wanawake, Kanisa Kuu Lushoto wametambua umuhimu wa mfuko wa maendeleo na kumuomba Mungu malengo na maono ya viongozi wa Dayosisi yapate kutimia kupitia mfuko huo.

Ibada hiyo iliyo ongozwa na  wanawake katika Kanisa Kuu Lushoto imeongozwa na Mwinjilisti Esther Mahimbo, na Mwenyekiti wa wenzi wa wachungaji kutoka KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Janeth Kalinga ndiye aliye hubiri neno la Mungu kutoka kitabu cha Mathayo 24:42-44.

Kwa upande mwingine Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru UEM kwa kuratibisha na kuwezesha warsha iliyo unganisha kundi kubwa na lililokamili la wake wa wachungaji na mashemasi kutoka KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani,katika warsha hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano SEKOMU.

Askofu Dkt. Msafiri Mbilu pia amewashukuru wake wa wachungaji kutoka Dayosisi ya Mashariki na Pwani kwa kutoa kiasi cha Tsh 500,000 (Mbegu) ili wake wa wachungaji na mashemasi waanzishe kikundi cha Vicoba ambacho, Baba Askofu ameahidi uongozi utasimamia kikundi hicho.

Mbali na kiasi hicho walicho kitoa wameweka alama ya kuimarisha undugu kati ya Dayosisi hizi mbili, katika vituo vya Dayosisi kama ifuatavyo.Shule ya Watoto wenye ulemavu wa akili Irente Tsh. 500,000, Kituo cha mafunzo na malezi bora kwa Watoto yatima Irente Tsh.500,000 pamoja na Tsh 500,000 kwaajili ya Shule ya wasioona Irente.