Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake, Katibu mtendaji wa idara ya mafunzo na uwezeshaji  kutoka UEM ,Mch Dkt. Andar Parlindungan mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe: 07/12/2022.

 UEM: United Evangelical Mission ni chama Cha kiinjili Cha kimisioni kilianzishwa mwaka 1996  na wamisionari kutoka Ujerumani wa Rhenish na Betheli ambao walifika Africa, na Asia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za Dini. Katika Africa walifika katika nchi 7 ambazo ni Tanzania, DR Congo, Africa ya Kusini, Botswana, Cameroon, Namibia na Rwanda kukiwa na madhehebu 15. Katika Tanzania inawakilishwa na Makanisa 4 ya KKKT ambayo ni KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na KKKT Dayosisi ya Karagwe.

Aidha Chama hiki chenye miaka 26 sasa kinashughulika katika nguzo tano ambazo ni Uhusiano/ Undugu, Diakonia, Uinjilishaji, Utetezi pamoja na Maendeleo.

KATIKA PICHA: Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu (wa tatu kutoka kulia), Katibu mtendaji wa idara ya mafunzo na uwezeshaji Mch Dkt. Andar Parlindungan (wa pili kutoka kulia), Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Kanju (wa kwanza kutoka kulia), Katibu Mkuu KKKT-DKMs Mwl. Julius Samwel Madiga (wa pili kutoka kushoto), Naibu Katibu Mtendaji wa UEM  Kanda ya  Africa Mch Dkt. Ernest William Kadiva (wa tatu kutoka kushoto pamoja na Mkurugenzi wa fedha na Utawala KKKT-DKMs CPA. Peter Singano.