KATIKA PICHA:Mkutano wa Maaskofu wote wa CCT na TEC uliofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye kituo cha Baraza la Maaskofu Catholic Tanzania tarehe 11-12/02/2025. Huu ni Mkutano wa Kitaifa wa CSSC (Christian Social Services Commission) ambao ulikuwa na mada Kuu ya kutathmini na kuona jinsi ya kuwa na mpango endelevu wa utoaji huduma bora za Elimu na Afya zinazotolewa na Makanisa nchini (Sustaining the provision of Quality Education and Health Care Services by the Churches in Tanzania).Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ni mmoja wa maaskofu walioshiriki mkutano huu.