Msaidizi wa Askofu toka KKKT Dayosisi ya Karagwe , Mch Yared A. Wakami yupo ziarani KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambapo leo tarehe 14/06/2021 ametembelea ofisi za wakuu wa majimbo ya Pwani na Tambarare.


.

Mch Yared Apolo Wakami  Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Karagwe

Awali akiwa katika Jimbo la Pwani alipata nafasi ya kutembelea Ofisi ya Mkuu wa Jimbo hilo Mch Thadeus A. Ketto iliyopo katika Usharika wa Kana, ambapo pia alitembelea kituo cha Mbuyu Kenda, Kana Center pamoja na Chuo cha Tanga Technical Institute. Baadae alifika katika Jimbo la Tambarare ambapo pia alipata nafasi ya kukutana na Mkuu wa Jimbo hilo Mch Frank Mntangi pamoja na watumishi wengine.

Katika ziara hii Mch Yared Apolo Wakami aliambatana na mwenyeji wake, msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Michael M. Kanju, amewatakia wakuu hao wa majimbo huduma njema na baraka tele za Mungu katika wajibu walioitiwa kuyaongoza majimbo hayo.

Mch Michael Mlondakweli Kanju Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

Tanga Technical Institute 

Mch Yared Wakami atakuwa katika Dayosisi yetu kwa juma moja, lengo likiwa ni kuendelea kujenga undugu, ushirikiano,kushirikishana uzoefu ,kuhamasisha na na kuitangaza UEM pamoja na kazi zote zinazofanywa na UEM. Aidha atashirikiana na msaidizi wa Askofu Mch Michael M. Kanju kufanya kazi za Injili na kutembelea miradi iliyofadhiliwa na UEM katika Dayosisi.

Ikumbukwe Mch Yared Wakami alishiriki katika Ibada ya kuwekwa jiwe la Msingi katika Usharika wa Kange mtaa wa Maweni tarehe tarehe12/06/2021 na Jana tarehe 13/06/2021 alishiriki Ibada iliyo kuwa na tendo la kuingizwa kazini kwa Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch Thadeus A.Ketto