TAARIFA KWA UMMA

Ofisi ya Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu inawaomba kupuuza ujumbe wa uzushi unaotumwa kwenye simu ukihusisha maneno yafuatayo.

Bwana yesu asifiwe mtumishi,upo wapi muda huu?.naomba unijibu kwa sms nipo kikaoni.ASK.DKT.MSAFIRI MBILU.

Mtu huyo mwenye namba 0693289600 anatumia jina la Askofu Dkt. Msafiri Mbilu kuomba hela na punde anapo jibiwa huandika.

Amen, naomba nikupe namba ya mtu unisaidie kumtumia elfu 40.nikitoka kikaoni nitakupa.

Askofu Dkt. Mbilu hajatuma ujumbe huo pamoja na kusikitishwa  na kitendo hiki  hivyo basi mnataarifiwa kupuuza ujumbe huo.