Print

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema kuwa elimu kwa vijana juu ya uandaaji na usimamizi wa miradi ni vema sasa ikatolewa katika Dayosisi nzima ili kuwa na vijana wenye uelewa wa kuandaa miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi na kuisaidia jamii.

Askofu Dkt.Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 23/07/2022 akiwa katika Usharika wa Muheza kwenye kilele cha mafunzo ya  muda mfupi ya uandaaji wa miradi,Tathimini Shirikishi ya Mafunzo (Participatory Learning Appraisal) pamoja na Upangaji wa mradi wenye muelekeo wa matokeo (Result Oriented Project ) yaliyoanza tarehe 11/07/2022 hadi tarehe 23/07/2022 yakijumuisha  vijana wapatao 16  wa Usharika huo.

Nimefurahi kwa Usharika,Washarika,Kamati ya miradi  kuwawezesha vijana hawa kupata mafunzo haya hasa kwenda vijijini kuona matatizo yalipo katika jamii kuandika miradi kwa wafadhili itakayo wapatia fedha zitakazo isaidia jamii, HILI NI JAMBO ZURI NALA KUPONGEZA. Alisema Askofu Mbilu.

Awali katika Ibada ya Jumuiya iliyo jumuisha jumuiya zote za Usharika huo iliyo ongozwa na Baba Askofu Dkt, Mbilu katika Usharika huo, amemshukuru Mkuu wa Jimbo la Tambarare Mch. Frank Mtangi, Mchungaji wa Usharika wa Muheza Mch. John Ndimbo wakufunzi pamoja na kamati mbalimbali zilizowezesha kufanikisha mafunzo hayo kwa vijana na kutoa wito kwa Majimbo na Sharika zingine kuiga jambo hilo.