Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  leo tarehe 12/06/2021 ameweka jiwe la msingi katika Usharika wa Kange mtaa wa Maweni.

Askofu Dkt Msafiri  Mbilu amewataka viongozi na washarika wa kanisa  kutumia majina ya asili ya sharika badala ya  kutumia  majina tofauti kutoka maeneo mengine  ili kutunza historia ya maeneo yao na Kanisa kwa ujumla.

Askofu Dkt Mbilu ameyasema hayo katika Usharika wa Kange mtaa wa Maweni Jimbo la Pwani Mkoani Tanga wakati akiweka jiwe la msingi la kanisa la KKKT DKMs Maweni ambapo amesema matumizi ya majina asili yatasaidia kutunza historia ya eneo husika tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo majina yamekuwa na mkanganyiko kutokana na kufanana na maeneo mengine.

Aidha Askofu Dkt Mbilu ameahidi kutoa mifuko 20 ya saruji ili kuendeleza ujenzi wa Kanisa hilo la maweni huku akiahidi kuendelea kushirikiana katika ujenzi wa Kanisa hilo huku akimpongeza Mchungaji Kiongozi wa usharika Mch. Emmanuel Mtoi pamoja na waumini wa Kanisa hilo kwa namna ambavyo wamejito kwa kushirikiana na viongozi wengine kuhakikisha ujenzi unaendelea, kiasi cha fedha hitajika ili kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo ya Ibada ni Tsh 120 M.

Katika Risala iliyosomwa Kanisani hapo wamesema kuwa ujenzi wa kanisa hilo umeaza mwaka 2011 na kugarimu kiasi cha shilingi Milioni 41 ambapo makisio yake ni million 60 huku mafanikio yakiwa ni Pamoja na washarika kuhamaisika kujitoa kwa ajili ya kanisa hilo kutokana na Kanisa la awali kuwa na nyufa jambo ambalo ilikuwa likihatarisha usalama wa waumini wao.

Kwa upande wao baadhi ya waumini wa mtaa huo wamewataka waumini wengine kuungana kwa pamoja katika ujenzi wa nyumba za Ibada badala ya kukimbilia katika makanisa ambayo yamekamilika na kurejea baada ya ujenzi kukamilika.

Askofu Dk Msafiri Mbilu kesho anategemea kumuingiza kazini mkuu wa jimbo mteule wa jimbo la Pwani Mch Thadeus A.Ketto Ibada itakayofanyika katika  Usharika wa kana kuanzia majira ya saa Mbili Asubuhi.

.............

Mch Michael Mlondakweli Kanju Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki 

Mch Yared Apolo Wakami  Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Karagwe

Pamoja na viongozi wengini wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki walio shiriki katika Ibada hii pia imehudhuriwa na Mch Yared Apolo Wakami  ambaye ni Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Karagwe. Mch  Yared Apolo Wakami    atakuwa katika Dayosisi yetu kwa juma moja lengo likiwa ni kuendelea kujenga undugu pamoja na kushirikishana uzoefu Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu amemkalibisha Mch Yared Apolo Wakami   Katika Dayosisi yetu.Ikumbukwe KKKT Dayosisi ya Karangwe inaongozwa na Baba Askofu Benson Bagonza.