TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI..

UTANGULIZI

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni miongoni mwa Dayosisi 27 ndani ya KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-DKMs ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi ifuatayo:

Sifa za waombaji ni kama ifuatavyo;

  1. DAKTARI DARAJA LA II (NAFASI 2)

Waombaji wawe na Shahada ya Udaktari wa binadamu kutoka Vyuo vikuu/ Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Waombaji wawe wamemaliza mafunzo ya kazi “internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika)

MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI.

  1. Awe raia wa Tanzania.
  2. Awe na umri usiopunguza miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato Cha Nne, Sita, Taaluma na usajili kamili (Full Registration) au leseni hai ya kufanya kazi ya taaluma husika.
  • Mwombaji aliyewahi kuajiriwa serikalini na kupata cheki namba, atatakiwa kuzingatia utaratibu wa kuomba kibali cha kurejea katika utumishi wa umma na kuendelea kutumia cheki namba baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye waraka na. CCB.228/271/01 wa tarehe 7 Agosti 2012.
  • Mwombaji awe na sifa na weledi kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya kama ilivyoainishwa hapo juu.
  • Waombaji wenye elemavu watapewa kipaumbele katika ajira hii kwa kuzingatia sheria ya watu wenye ulemavu Na. 1 ya mwaka 2010.

MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA,

  1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  2. Nakala ya cheti cha kidato cha nne au/ na cha sita au stashahada kulingana na kada ya mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje ya nchi waambatanishe cheti cha ithibati kutoka baraza la mitihani Tanzania (NECTA).
  • Nakala ya vyeti vya Taaluma na Transcript, Aidha waliosoma vyuo vya nje ya nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU.
  1. Wasifu (CV).
  2. Nakala ya cheti cha Usajili na Leseni hai ya taaluma husika (Full Registration & Valid Licence).
  3. Nakala ya cheti cha Mafunzo kwa vitendo (Internship).
  • Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
  • Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA/ Namba ya NIDA).
  1. Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako Pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa viapo na kusajiliwa na Msajili wa hati, wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.

Maombi yote yatumwe ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe: 06/06/2023)Maombi yote yatumwe kwa Ofisi ya Katibu Mkuu-KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki S.L.P 10 LUSHOTO Au: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.