ELCT North Eastern Diocese
Wakristo wa KKKT kutoka Ngorongoro wapokelewa rasmi KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt. Solomon Jacobo Massangwa amemshukuru na kumpongeza Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, kwa kukubali kuwapokea washarika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania waliohama kutoka KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Enndulen-Ngorongoro na kuhamia KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki katika Jimbo la Tambarare Usharika wa Handeni Mtaa wa Msomera.
- Hits: 5463
Askofu Dkt. Msafiri Mbilu atoa wito kwa Kanisa kuwatambua viziwi
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ametoa wito kwa wachungaji na watumishi wengine wa Kanisa kuwatambua watu wenye shida ya kusikia (viziwi) ili wasiachwe na ujumbe wa neno la Mungu unapohubiriwa.
- Hits: 4975
Katibu Mkuu mpya wa KKKT-DKMs atambulishwa Jimbo la Pwani Usharika wa Kange.
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amemtambulisha Katibu Mkuu Mpya wa KKKT-DKMs Mwl. Julius Samweli Madiga kwa Washarika wa Jimbo la Pwani hususani wa Usharika wa Kange.
- Hits: 5457
Askofu Dkt. Mbilu akutana na Katibu mtendaji wa idara ya mafunzo na uwezeshaji wa UEM
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake, Katibu mtendaji wa idara ya mafunzo na uwezeshaji kutoka UEM ,Mch Dkt. Andar Parlindungan mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe: 07/12/2022.
UEM: United Evangelical Mission ni chama Cha kiinjili Cha kimisioni kilianzishwa mwaka 1996 na wamisionari kutoka Ujerumani wa Rhenish na Betheli ambao walifika Africa, na Asia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za Dini. Katika Africa walifika katika nchi 7 ambazo ni Tanzania, DR Congo, Africa ya Kusini, Botswana, Cameroon, Namibia na Rwanda kukiwa na madhehebu 15. Katika Tanzania inawakilishwa na Makanisa 4 ya KKKT ambayo ni KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na KKKT Dayosisi ya Karagwe.
Aidha Chama hiki chenye miaka 26 sasa kinashughulika katika nguzo tano ambazo ni Uhusiano/ Undugu, Diakonia, Uinjilishaji, Utetezi pamoja na Maendeleo.
KATIKA PICHA: Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu (wa tatu kutoka kulia), Katibu mtendaji wa idara ya mafunzo na uwezeshaji Mch Dkt. Andar Parlindungan (wa pili kutoka kulia), Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Kanju (wa kwanza kutoka kulia), Katibu Mkuu KKKT-DKMs Mwl. Julius Samwel Madiga (wa pili kutoka kushoto), Naibu Katibu Mtendaji wa UEM Kanda ya Africa Mch Dkt. Ernest William Kadiva (wa tatu kutoka kushoto pamoja na Mkurugenzi wa fedha na Utawala KKKT-DKMs CPA. Peter Singano.
- Hits: 5632
Page 35 of 107