ELCT North Eastern Diocese
Mkuu mpya wa Kanisa la Sweden Askofu Dkt. Martin Modéus aingizwa kazini.
- Details
Leo tarehe 04/12/2022 Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameendelea na ziara yake nchini Sweden katika mji wa Uppsala (Cathedral) na ameshiriki kwenye Ibada ya kuingizwa kazini kwa Mkuu mpya wa Kanisa la Sweden (The Church of Sweden), Askofu Dkt. Martin Modéus.
Askofu Dkt. Mbilu ambaye pia amemuwakilisha Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo kwenye Ibada hiyo.
Mkuu wa KKKT anakupongeza sana kwa kuchaguliwa na kuingizwa kazini kuwa Mkuu mpya wa Kanisa la Sweden.Tunakutakia baraka tele za Mungu wakati huu wa kusimikwa kwako kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Sweden.
“Mungu wetu akupe nguvu na hekima zote katika wajibu huu mkuu ulioupokea leo. Ni maombi na matumaini yetu kwamba urafiki na ushirikiano wetu wa muda mrefu na mzuri utaendelea chini ya uongozi wako. Sisi wa KKKT tunakuahidi kukuombea na kukupa ushirikiano wa kutosha.
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso” (Zaburi 46:1).
Ibada hiyo imehudhuriwa na Maaskofu kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo, Norway, Finland, Denmark, USA, Tanzania pamoja na Ethiopia. Pia Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF), Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa Duniani (WCC) pamoja na Präses wa Kanisa la Westphalia (EKD) Annette Kurschuss ni miongoni mwa watu walioshiriki katika Ibada hiyo.
Askofu Martin Modéus alipata asilimia 59 ya kura katika uchaguzi wa Askofu Mkuu uliofanyika tarehe 08/06/2022 hivyo amekuwa Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Sweden, akimrithi mtangulizi wake Askofu Antje Jackelen, ambaye alistaafu tarehe 30 Oktoba ya mwaka huu.
Askofu Modéus anakuwa Askofu Mkuu wa 71 wa Kanisa hilo katika mlolongo usiokatika tangu Askofu Mkuu wa kwanza, Askofu Stephanus, mwaka 1164.
- Hits: 5729
Matukio katika picha Ofisi Kuu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details
Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mchungaji Michael Mlondakweli Kanju (watatu kutoka kushoto) akiwa na wachungaji waliomaliza mafunzo yao ya CPE (Clinical Pastoral Education) katika Chuo cha KCMC-Moshi.
Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Mlondakweli Kanju, Mch. Godfrey Walalaze Katibu Mkuu aliyemaliza muda wake,Wakurugenzi na baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu wakiwa katika zoezi la kumkabidhi Ofisi Katibu Mkuu mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Samwel Madiga leo tarehe 30/11/2022.
- Hits: 6654
Askofu Dkt. Mbilu ziarani nchini Sweden yenye lengo la kutoa fursa ya kukuza uhusiano na urafiki
- Details
Katika picha Askofu Dkt. Msafri Joseph Mbilu, akiwa na mwenyeji wake Askofu Johan Tyrberg. Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu yupo ziarani katika Dayosisi ya Lund-Sweden, ziara hii ni mwendelezo wa ziara zake ndani na nje ya nchi zenye lengo la kuimarisha urafiki pamoja na kujifunza mambo mbalimbali na mengi yatakayo faa kwa ajili ya Dayosisi na Kanisa.
KATIKA PICHA: Sehemu ya msafara ulioambatana na Askofu Dkt. Msafiri Mbilu
Askofu Dkt. Mbilu atapata nafasi ya kutoa taarifa mbalimbali juu ya urafiki na hali ya Dayosisi kwa sasa katika sharika na vituo mbalimbali, atahutubia katika Chuo Kikuu cha Lund (Lund University), pamoja na kukutana na watumishi wa Kanisa na wachungaji. Ziara hii ya Askofu Dkt. Mbilu inatoa fursa ya kukuza uhusiano na urafiki kati ya Dayosisi hizi.
Askofu Martin Modéus
Jumapili ya tarehe 04/12/2022 Askofu Dkt. Mbilu atamuwakilisha Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo kwenye Ibada ya kuingizwa kazini kwa Mkuu mpya wa Kanisa la Sweden, Askofu Martin Modéus.
Askofu Martin Modéus alipata asilimia 59 (59%) ya kura katika uchaguzi wa Askofu Mkuu uliofanyika tarehe 08/06/2022. Hivyo atakuwa Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Sweden, akimrithi mtangulizi wake Askofu Antje Jackelen, ambaye alistaafu tarehe 30 Oktoba ya mwaka huu. Askofu Modéus ataingizwa kazini kuwa Askofu Mkuu mpya tarehe 4 Desemba 2022.
Askofu Modéus anakuwa Askofu Mkuu wa 71 wa Kanisa la Sweden katika mlolongo usiokatika tangu Askofu Mkuu wa kwanza, Askofu Stephanus, mwaka 1164. Askofu Martin Modéus kwa sasa ni Askofu wa Dayosisi ya Linköping.
Ujumbe wa Askofu huyu mpya wa Kanisa la Sweden "Ninashukuru na nina furaha ninatazamia kutekeleza majukumu yangu, kwa msaada wa Mungu na kwa msaada wa wenzangu wazuri na wafanyikazi. Sasa ni wakati wa maandalizi, tafakari na maombi kabla ya kuingizwa kazini,” alisema Askofu Martin Modéus mara baada ya kupokea wajibu huo.
- Hits: 6031
Katibu Mkuu mpya wa KKKT-DKMs, Mwl. Julius Madiga awasili Makao Makuu wa Dayosisi
- Details
Leo tarehe 21/11/2022 Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Samweli Madiga, ametambulishwa rasmi kwa wafanyakazi wa Ofisi Kuu ya KKKT-DKMs ambapo pia amepata nafasi ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Askofu. Atakua bega kwa bega na aliyekuwa Katibu Mkuu Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa muda wa mwezi mmoja kama moja ya taratibu ya kukabidhiana Ofisi.
KATIBU MKUU KKKT-DKMs, MWL. JULIUS SAMWELI MADIGA.
- Hits: 9159
Page 36 of 107