ELCT North Eastern Diocese
Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo afungua mafunzo ya siku mbili yanayohusu utoaji wa huduma bora za Afya
- Details
MKUU WA KKKT BABA ASKOFU DKT. FREDRICK ONAEL SHOO.
Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo leo tarehe 18/10/2022, amefungua mafunzo ya siku mbili yanayohusu utoaji wa huduma bora za Afya katika Hospitali na vituo vya Afya vinavyo milikiwa na KKKT.
Mafunzo haya yanafanyika Jijini Dodoma ambapo yamehudhuriwa na wajumbe kutoka Hospitali 23 na vituo vya Afya 24 vya KKKT. Wajumbe hao ni pamoja na maaskofu, makatibu wakuu pamoja na wataalamu wa Afya.
- Hits: 5903
Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu awashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa namna walivyo jitoa kwa hali na mali katika kufanikisha uzinduzi wa Dayosisi ya Magharibi.Shukrani hizo amezitoa leo tarehe 16/10/2022 wakati akihubiri kwenye Ibada ya Jumapili iliyofanyika katika Jimbo la Kusini Usharika wa Bumbuli.
- Hits: 6888
Askofu Dkt. Mbilu aongoza Maombi ya kumshukuru Mungu kwaajili ya kufunguliwa kwa Chuo cha KOTETI
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 15/10/2022 akiwa katika Jimbo la Kaskazini Usharika wa Kireti Mtaa wa Mp'anda, ameongoza maombi maalum ya kumshukuru Mungu kufuatia kufunguliwa kwa Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kinacho milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Hits: 6404
Page 37 of 105