ELCT North Eastern Diocese
Ibada ya mazishi ya Mama Damaris Appelesy Ketto
- Details
Askofu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,leo tarehe 18/01/2022 ameongoza Ibada ya mazishi ya marehemu Mama. Damaris Appelesy Ketto,mama mzazi wa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch Thadeus A. Ketto ,
Ibada hiyo imefanyika katika Usharika wa Mtonga jimbo la tambarare.marehemu Mama. Damaris Appelesy Ketto aliitwa mbinguni jioni tarehe 14/01/2022. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
- Hits: 7360
Pumzika kwa amani Mama, DAMARIS APPELESY KETTO
- Details
Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio,wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza , yamekwisha kupita UFUNUO 21:4.
Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mama. Damaris Appelesy Ketto,mama mzazi wa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch Thadeus A. Ketto ,kilichotokea jana Ijumaa tarehe 14/01/2022.Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Jumanne tarehe 18/01/2022 katika Kanisa la KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Mtonga - Korogwe. Uongozi unatoa pole kwa Mkuu wa Jimbo la Pwani, Mch. Thadeus A. Ketto, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe
- Hits: 8231
Ibada ya Jumapili KKKT-DKMs Usharika wa Duga
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 09/01/2022 ameongoza Ibada ya jumapili katika Usharika wa Duga Jimbo la Pwani.awali Baba Askofu aliweka jiwe la msingi katika nyumba ya mtumishi.Liturgia katika Ibada hiyo iliongozwa na mkuu wa Jimbo la Pwani Mch.Thadeus A. Ketto.
Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti,Mashemasi,Kwaya,Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Duga.
- Hits: 8260
Ibada ya Jumapili Usharika wa Mbaramo Mtaa wa Mlesa
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt.Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 02/01/2022 ameongoza Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Mbaramo Mtaa wa Mlesa, Imekuwa siku ya Baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mbaramo mtaa wa Mlesa. Ibada hiyo ilikuwa na matukio mbalimbali ikiwemo uwekwaji wa jiwe la msingi katika nyumba ya mtumishi pamoja na kufunguliwa kwa mnara wa kengele.
- Hits: 8050
Page 62 of 107