ELCT North Eastern Diocese
Majibu juu ya zilipo fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Dayosisi kupatikana.
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu kama msimamizi wa mali za Dayosisi kupitia halmashauri Kuu ambayo yeye ni mwenyekiti wake amesema kuwa watahakikisha majibu ya zilipo fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Dayosisi ambazo hazikutumika kama ilivyokusudiwa yanapatikana.
Katika kufanikisha hilo amesema kuwa watumishi mbalimbali ikiwemo wachungaji waliokuwa wakiwajibika kusimamia fedha hizo wataulizwa hata ikibidi kwa ukali.
- Hits: 8446
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Mgwashi Jimbo la Kusini
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 21 Novemba, 2021 ameongoza Ibada ya Kipaimara katika Usharika wa Mgwashwi, Jimbo la Kusini.
Imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mgwashwi ambapo jumla ya vijana wapatao 140 walibarikiwa na wawili kati yao walibatizwa.
Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu amewakumbusha vijana hao walio barikiwa kutokuondoka katika kweli ya neno la Mungu na kamwe wasiyumbishwe na mafundisho potofu ya neno la Mungu yaliyo kisiri katika nyakati hizi.
- Hits: 9106
Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs, Mch Michael Mlondakweli Kanju afungua Kongamano la Maombi na Maombezi
- Details
Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju ameupongeza uongozi wa kituo cha Redio Utume Fm chini ya Kaimu meneja wa kituo hicho Bi. Evelyne Balozi Mariki kwa kuendeleza maono ya Dayosisi ya kueneza Injili kwa wote.
- Hits: 8130
Page 68 of 107