ELCT North Eastern Diocese
Mratibu wa Mawasiliano wa KKKT, atembelea Makao Makuu ya KKKT-DKMs
- Details
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo na Mratibu wa Mawasiliano wa KKKT, ndugu Erick Adolph ambae ametembelea Makao Makuu ya KKKT-DKMs leo tarehe 19 Novemba, 2021.
- Hits: 7996
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Vuga Jimbo la Kusini
- Details
Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;Nitakushauri,jicho langu likikutazama.
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amewataka viongozi walio pewa dhamana ya kusimamia mali za Dayosisi kuendelea kuwa mawakili wema kwa kufanya kazi kwa uamainifu, uadilifu na uwazi kwakuwa wameaminiwa na yeyeto atakayefanya tofauti lazima ataulizwa.
- Hits: 9256
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Kana, Youths Confirmation at Kana Lutheran Parish
- Details
“……Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.”
Leo tarehe 07/11/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Usharika wa Kana, Jimbo la Pwani, ambapo vijana wapatao 33 walibarikiwa na mmoja kati yao alibatizwa.
- Hits: 10174
TANZIA-
- Details
"Naye atafuta kila chozi katika macho yao,wala mauti haitakuwepo tena,wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita " UFUNUO 21:4.
Kaimu Katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya Uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki anasikitika kutangaza kifo cha Mama Mzazi wa Mch.Juliana Mahundo, Bi. Raheli Mahundo, kilichotokea tarehe 05/11/2021.
Ibada ya mzishi itafanyika siku ya Jumatatu tarehe 08/11/2021katika mtaa wa Mindu, Usharika wa Kwabada-Muheza.
Uongozi unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
- Hits: 7831
Page 69 of 107