ELCT North Eastern Diocese
Salamu za Pole
- Details
......................................................................................................................
Jeneza lenye Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ukiwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay
- Hits: 13603
Matukio katika picha Mkutano Mkuu maalumu wa KKKT-DKMS
- Details
Mkutano Mkuu maalumu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kwa siku ya pili leo Machi 12, 2021 kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa katika Chuo cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU.
- Hits: 11604
MWANGAZA Educational Center program Coordinators watembelea Ofisi za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Details
Mwangaza program coorinators leo tarehe 10/03/2021 wamepata nafasi ya kutembelea Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki lengo likiwa ni kutembelea shule za sekondari za Dayosisi.
Katika picha ni ,Mwl.John Kavishe wa kwanza kutoka kushoto,Mr.Richard Mbwambo wa pili kutoka Kushoto,Mch.Joyce Kibanga Mkurugenzi wa huduma za jamii wa tatu kutoka kushoto na Bi.Salome Lally wa nne kutoka kushoto. Kutoka kulia ni Bw. David Chanyeghea Kaimu Mkurugenzi Uchumi,Mipango na Maendeleo, Kaimu Katibu Mkuu Mch.Godfrey Walalaze wa pili kutoka kulia, Dean Mteule Mch. Michael Kanju wa tatu kutoka kulia na Askofu. mteule Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu wa tano kutoka kulia.
- Hits: 11111
KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki yafanya Uzinduzi wa Harambee kubwa yenye lengo la kuimarisha Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU.
- Details
Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amejumuika na Washarika wa Usharika wa Kana katika Ibada ya Jumapili ambapo Ibada hiyo pamoja na kuwa na matukio mbalimbali kumekuwa na Uzinduzi wa Harambee yenye lengo la kuchangisha jumla ya Sh 2,000,000,000 (Bilioni Mbili) ili kuimarisha Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU.
Katika Hotuba yake aliyoitoa kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela, Askofu Mteule Mch.Dkt. Mbilu alisema imekuwa siku ya furaha kubwa kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo alimkaribisha Mkuu huyo wa Mkoa katika Usharika wa Kana na Dayosisi kwa ujumla.
Askofu Mteule Mch.Dkt. Mbilu amesema kuwa katika kipindi cha takribani miaka 3 kumekuwa na changamoto kubwa ya Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU, kufungiwa udahili kutoka na matatizo mbalimbali ya kimfumo na yaki utendaji.Hata hivyo baada ya Uongozi mpya wa Dayosisi kuingia madarakani mwezi Novemba 2020 uongozi umejikita sana katika kuhakikisha Chuo Kikuu cha SEKOMU kinasimama tena.
- Hits: 13178
Page 106 of 124