ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI MOJA YA KAZI MENEJA WA SHAMBA (FARM MANAGER) KITUO CHA IRENTE FARM

    TANGAZO LA NAFASI YA KAZI Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya...
  • Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji  NSSF

    Askofu Dkt.Mbilu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Uendeshaji NSSF

    Leo tarehe 01/04/2026, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amepokea ugeni kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifa...
  • TAARIFA

    TAARIFA

    Uongozi wa KKKT – Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ukiwakilishwa na Katibu Mkuu Mwl. Julius Madiga, u...
  • ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    ASKOFU KKKT DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI AZINDUA BODI YA MFUKO WA PENSION

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Dkt. Msafiri Jos...
  • Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Taarifa Ziara ya Botswana kwenye Mkutano wa UEM Kanda ya Afrika

    Dayosisi yetu imepata heshima kubwa ya kushiriki katika Mkutano wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na U...

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Mkutano wa Maaskofu wote wa CCT na TEC

  • Print
Details
Published: 11 February 2025

KATIKA PICHA:Mkutano wa Maaskofu wote wa CCT na TEC uliofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye kituo cha Baraza la Maaskofu Catholic Tanzania tarehe 11-12/02/2025. Huu ni Mkutano wa Kitaifa wa CSSC (Christian Social Services Commission) ambao ulikuwa na mada Kuu ya kutathmini na kuona jinsi ya kuwa na mpango endelevu wa utoaji huduma bora za Elimu na Afya zinazotolewa na Makanisa nchini (Sustaining the provision of Quality Education and Health Care Services by the Churches in Tanzania).Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ni mmoja wa maaskofu walioshiriki mkutano huu.

Hits: 7948

Read more ...

Wakristo watakiwa kutenga muda kutulia Nyumbani mwa Bwana

  • Print
Details
Published: 09 February 2025

 HABARI KWA UFUPI

Wakristo wamekumbushwa kuendelea kumtumaini na kumtegema Mungu pale wanapo pata mafanikio katika maisha yao kwani katika dunia ya sasa wapo waliofanikiwa na mara baada ya kupata mafanikio hayo wakamsahau Mungu na kufuata njia zao, na kuamini kuwa mafanikio hayo wameyapata kwa nguvu zao.

Hits: 7722

Read more ...

Pumzika kwa Amani Bibi. Elise David Ngome

  • Print
Details
Published: 28 January 2025
Ufunuo 14:13“Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
 
KATIKA PICHA:Ibada ya mazishi ya Bibi. Elise David Ngome, iliyofanyika leo tarehe 28/01/2025 katika Jimbo la Kusini Usharika wa Mgwashi na kuongozwa na msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Michael Mlondakweli Kanju akishirikiana na Mkuu wa Jimbo la Kusini Mch. Issai Mweta.
Hits: 7525

Read more ...

Matokeo kidato cha nne Shule ya Lwandai na Bangala zafanya vizuri Askofu Dkt. Mbilu asema zimewapa raha wana KKKT-DKMS

  • Print
Details
Published: 23 January 2025

Shule za Sekondari za Lwandai na Bangala Junior Seminary, zinazomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), zimeendelea kufanya vizuri katika matokeo  ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika November, 2024

 Katika matokeo hayo, shule ya Lwandai imevutia zaidi baada ya kutoa mwanafunzi aliyepata alama za juu akiwa na daraja la kwanza lenye pointi saba (One ya 7), kitu kinachoashiria uwekezaji mkubwa katika elimu bora na juhudi za walimu pamoja na wanafunzi.

  Kufuatia matokeo hayo Askofu wa KKKT-DKMs, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ,ametoa pongezi kwa walimu na wafanyakazi wa Shule hizo kwa kazi nzuri walioifanya huku akiahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kuweka msingi imara wa mafanikio zaidi ya siku zijazo.

 Kakita hatua nyingine Askofu Dkt. Mbilu, ametoa shukrani zake za dhati kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Dayosisi kwa kukubali ombi la kila Usharika wa KKKT-DKMS kusomesha mwanafunzi mmoja katika Shule hizi.

 “ninapoyatazama matokeo haya ya kishindo ya Shule zetu Lwandai na Bangala ninajikuta mdomo wazi nikimshangaa Mungu kwa jambo hili kubwa alilotutendea. Ninawapongeza ninyi wote kwa maamuzi yale magumu tuliyofanya kwenye kikao chetu cha kwanza cha tarehe 17.12.2020 kuwa kila Usharika usomeshe mwanafunzi mmoja kuanzia Januari 2021 ili kuondoa aibu ya Shule hizi kuwa na wanafunzi wachache wa kidato cha kwanza Lwandai 8 na Bangala 3. Hili limezaa matunda haya na kwa hakika Shule zetu zimefufuka. Hongereni sana.

 Siku chache kabla ya Mtihani wa kidato cha Nne nilitembelea Shule zetu hizi kufanya maombi na watoto wetu na kuwapa kila mmoja kalamu ya kufanyia Mtihani kwa niaba yenu. Hakika Mungu amesikia maombi yetu na ametenda na ameamua KUTUPA RAHA. Nawapongeza ninyi Wajumbe wa Halmashauri Kuu, Wana KKKT-DKMS na wadau wote wa maendeleo  kwa Ufadhili wao.

Nawapongeza Wazazi wa watoto hawa, Nawapongeza Wakuu wa Shule zetu, Walimu wote na watenda kazi wote kwa ufaulu huu wa hali ya juu sana. Tunazo hadi Divisheni One ya point 7. Nawapongeza watoto wetu kwa kufanya vizuri kwenye Mtihani Huu”Amesema Askofu Dkt. Mbilu.

 Pamoja na hayo Askofu Dkt. Mbilu, amempogeza kipekee mwanafunzi Helena Frank Kaduma wa shule ya sekondari Lwandai kwa kupata ufaulu wa Division One ya point 7 ambapo mwanafunzi huyo amesomeshwa na Usharika wa Hale pamoja na mwanafunzi kutoka shule ya seminari ndogo ya Kilutheri Bangala,Dickson David Kika ambaye amepata ufaulu wa Division one ya 9 ambaye amesomeshwa na usharika wa Soni.

Matokeo haya mazuri yanaendeleza sifa nzuri ya shule hizi kama vituo vya elimu vinavyozalisha viongozi wa kesho walio na maarifa na maadili mema, na ujuzi unaohitajika kwa maendeleo ya Taifa. Sharika za KKKT-DKMS zitaendelea kuwasomesha vijana hawa kidato cha Tano na cha Sita. Mungu aendelee kutubariki tunapoyafanya makubwa haya. "BWANA AKASEMA, USO WANGU UTAKWENDA PAMOJA NAWE, NAMI NITAKUPA RAHA"(Kutoka 33:14).

Hits: 8081
  1. Uanzishwaji wa kozi ya muziki KOTETI maandalizi yanaendelea vizuri
  2. Kuelekea Ibada ya kuwekwa wakfu Askofu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria (Mwanza)
  3. Picha ya pamoja mara baada ya Mkutano wa Halmashauri ya Utumishi ya KKKT
  4. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi aitembelea KKKT-DKMs

Page 13 of 137

  • 8
  • 9
  • ...
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • ...
  • 16
  • 17

Back to Top

© 2026 ELCT North Eastern Diocese