ELCT North Eastern Diocese
Toggle Navigation
  • Home
  • Our Diocese
  • Wopa
  • Gallery
  • Institutions
    • Irente Children's Home
    • Irente School for the Blind
    • Rainbow School
    • Lwandai Secondary School
    • Lutindi Mental Hospital
    • Bangala Lutheran Junior Seminary
    • Bumbuli Hospital
    • SEKOMU university
    • Namna ya kuchangia kazi za maendeleo na Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye mahitaji maalumu (KKKT-DKMs)
  • Calendar
  • Projects
    • Irente Biodiversity Reserve
    • UTC - Usambara Technological Center
    • Restaurants and Hostels
      • Tumaini Mbuyukenda Hostel and Restaurant
      • Martin Luther Garden and Restaurant
      • Tumaini Songe Restaurant and Hostel
      • Hohen Restaurant and Hostel
      • Tumaini Lushoto Restaurant and Hostel
  • Superintendent
    • Coast Superintendent
    • Northern Superintendent
    • Southern Superintendent
    • Plains Superintendent
  • New-clips
  • Contact us
  • You are here:  
  • Home

Bishop Rev.Dr. Msafiri J. Mbilu

Change Language

English German Spanish Swahili Swedish

News & Updates

  • Uongozi Bora: Askofu Dkt. Mbilu Aweka Mkazo kwenye Stahiki za Watumishi wa Dayosisi

    Uongozi Bora: Askofu Dkt. Mbilu Aweka Mkazo kwenye Stahiki za Watumishi wa Dayosisi

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), Dkt...
  • Mtheolojia Steven Emanuel Mhangwa abarikiwa kuwa Mchungaji

    Mtheolojia Steven Emanuel Mhangwa abarikiwa kuwa Mchungaji

    Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki(KKKT-DKMs), Dkt....
  • KATIKA PICHA NI MATUKIO YA IBADA YA KUBARIKIWA WACHUNGAJI KKKT-DKMs

    KATIKA PICHA NI MATUKIO YA IBADA YA KUBARIKIWA WACHUNGAJI KKKT-DKMs

    Matukio katika picha ni Ibada ya Jumapili siku ya Bwana ya 2 Kabla ya Majilio iliyofanyika KKKT-Dayo...
  • Pumzika kwa Amani Mwl. Mwanga  Yona  Wetundwa

    Pumzika kwa Amani Mwl. Mwanga Yona Wetundwa

  • Mwendelezo wa Ziara ya Askofu Johan Tyrberg

    Mwendelezo wa Ziara ya Askofu Johan Tyrberg

.



 

 

Staff Email

ELCT North Eastern Diocese

Uongozi Bora: Askofu Dkt. Mbilu Aweka Mkazo kwenye Stahiki za Watumishi wa Dayosisi

  • Print
Details
Published: 28 November 2025

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs), Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ametoa pongezi za dhati kwa Wainjilisti Wanaume wa Dayosisi kwa huduma yao na uaminifu katika kuitenda kazi shambani mwa Bwana.

Akizungumza tarehe 28/11/2025 wakati akifungua semina maalum inayowakutanisha Wainjilisti wanaume wa KKKT-DKMs katika Usharika wa Korogwe, Askofu Dkt. Mbilu alisisitiza kuwa uongozi wa Dayosisi unatambua, kuthamini na kulinda mchango muhimu wa Wainjilisti katika kukuza na kuimarisha kundi la Mungu.

Aliongeza kuwa nguvu, hekima na kujitoa kwao kunaleta matokeo na ustawi si tu katika Kanisa bali hata katika jamii wanazozihudumia.

Kwa msisitizo wa kipekee Askofu Dkt. Mbilu ameonesha moyo wake wa kujali watumishi kwa kubainisha kuwa ataendelea kusimamia kwa karibu masuala yote yanayohusu ustawi na haki za watumishi wote katikadayosisi.

Ameahidi kuhakikisha stahiki mbalimbali zinaendelea kutolewa kwa wakati, ikiwemo michango ya NHIF na mifuko mingine ya kijamii, ili watumishi waendelee kufanya kazi kwa amani, uadilifu na matumaini huku akiitaka Ofisi ya Msaidizi wa Askofu kutoa mapema taarifa katika Ofisi ya Askofu punde Wainjilisti wanapokaribia kustaafu.

Askofu Dkt. Mbilu amesisitiza kuwa uongozi hauishii katika kuongoza tu, bali unajumuisha pia kuhakikisha kuwa wale wanaohudumu katika nafasi mbalimbali katika Dayosisi wanatunzwa, wanathaminiwa na kuwekewa mazingira bora ya kutekeleza huduma ikiwa hii ni sehemu ya wito wa Kristo wa kujenga, kuenzi na kutiana nguvu katika kuitenda kazi ya Bwana.

Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii
INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV
WEBSITE: www.elctned.org
KWA MAONI NA USHAURI:
Simu : +255 743 399 798

Hits: 481

Mtheolojia Steven Emanuel Mhangwa abarikiwa kuwa Mchungaji

  • Print
Details
Published: 22 November 2025

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki(KKKT-DKMs), Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, ameongoza Ibada ya kumbariki na kumuingiza kazini Mtheolojia Steven Emanuel Mhangwa kuwa Mchungaji, leo 22/11/2025, katika Jimbo la Pwani, Usharika wa Kange.

Awali, Mch. Steven Mhangwa alipaswa kuwa miongoni mwa watheolojia 14 waliobarikiwa kuwa Wachungaji katika Ibada ya Jumapili ya Siku ya Bwana ya 2 Kabla ya Majilio, iliyofanyika katika Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto tarehe 16/11/2025. Hata hivyo, kutokana na sababu za kiafya, amebarikiwa leo tarehe 22/11/2025.

Hits: 783

Read more ...

KATIKA PICHA NI MATUKIO YA IBADA YA KUBARIKIWA WACHUNGAJI KKKT-DKMs

  • Print
Details
Published: 16 November 2025
Matukio katika picha ni Ibada ya Jumapili siku ya Bwana ya 2 Kabla ya Majilio iliyofanyika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto.tarehe 16/11/2025.
 
Ibada hii iliongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu akishirikiana na watumishi wengine na iliambatana na tendo la Kubarikiwa watheologia 14 kuwa Wachungaji ambao ni.
Hits: 930

Read more ...

Mwendelezo wa Ziara ya Askofu Johan Tyrberg

  • Print
Details
Published: 27 September 2025

 

Hits: 1998

Read more ...

  1. Pumzika kwa Amani Mwl. Mwanga Yona Wetundwa
  2. Pumzika kwa Amani Mchungaji Yohana Vicent Titu
  3. TANGAZO LA NAFASI YA KAZI MRATIBU WA HUDUMA YA MTOTO NA KIJANA KKKT – MKATA – TZ1211
  4. Tangazo la kazi Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Mtoto TZ1211 MKATA-HANDENI

Page 1 of 132

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • ...
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10

Back to Top

© 2025 ELCT North Eastern Diocese