Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Latest Posts

Miaka 5 ya Askofu wa KKKT-DKMs Dkt. Msafiri Joseph Mbilu

Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Uongozi wa Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki tarehe 09/05/2026 kuelekea mageuzi, Kutoka “kujenga misingi” kwenda ubora wa juu .

SAFARI YA MAGEUZI, UMOJA NA UTHABITI WA IMANI.

Katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ndani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, kumeshuhudiwa mageuzi makubwa ya kiroho, kiutawala na kijamii. Uongozi wake umejikita katika umoja, uwajibikaji, uadilifu na maono ya kulijenga kanisa linalojitegemea na kumhudumia mwanadamu kwa ukamilifu wake.

Moja ya mafanikio makubwa ni kuimarika kwa umoja ndani ya dayosisi. Kupitia mikutano ya mara kwa mara, mafundisho ya upendo na mshikamano, migawanyiko iliyowahi kujitokeza imepungua kwa kiasi kikubwa. Umoja huu umeonekana si tu katika Ibada, bali pia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.

Katika kipindi hiki pia, imani ya wadau na serikali imerejea. Uongozi wa Askofu Dkt.Mbilu umeweka mkazo katika uwazi wa matumizi ya rasilimali na usimamizi bora wa miradi. Hali hii imeifanya dayosisi kuwa mshirika anayeaminika katika sekta za elimu, Afya na ustawi wa jamii.

Katika kulinda misingi ya imani, Askofu Dkt.Mbilu ameweka kipaumbele katika mafundisho sahihi ya Neno la Mungu. Ameimarisha mafunzo kwa wachungaji na wahubiri, jambo lililochangia ukuaji wa kiroho wa waumini na kulinda Kanisa dhidi ya mafundisho potofu.

Huduma za diakonia zimepata nguvu mpya, zikilenga zaidi kuwahudumia wenye uhitaji maalum wakiwemo yatima, wajane na watu wenye ulemavu. Aidha, uwekezaji katika elimu na Afya umeboreshwa kwa kiwango kikubwa kupitia taasisi za Kanisa.

Vijana nao hawakuachwa nyuma. Askofu Dkt.Mbilu ameweka mazingira ya kuwawezesha kushiriki katika uongozi na huduma, ikiwa ni pamoja na kuanzisha programu za ujasiriamali na matumizi ya teknolojia katika uinjilisti.

Katika eneo la utawala, dayosisi imeimarisha mifumo ya utawala bora, mipango mkakati na tathmini endelevu. Hii imeongeza ufanisi na kutoa mwelekeo ulio wazi wa maendeleo.

Moja ya mafanikio makubwa na ya kihistoria ni kupungua kwa deni la dayosisi kutoka takribani shilingi bilioni 7.6 hadi kufikia bilioni 2.3 ndani ya miaka mitano. Mafanikio haya ni matokeo ya mshikamano, nidhamu ya kifedha na ushirikiano wa wadau mbalimbali.

Kihistoria, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alichaguliwa kuwa Askofu tarehe 26 Novemba 2020 kwa kupata asilimia 89.4 ya kura, na kuingizwa rasmi kazini tarehe 9 Mei 2021 akiwa Askofu wa tano wa dayosisi hiyo. Safari yake ya uongozi imekuwa ushuhuda wa maono, uthabiti na kujitoa kwa dhati.

Leo, Mei 9, 2026, ikiwa ni miaka mitano tangu aingie madarakani, Askofu Dkt.Mbilu anatoa shukrani kwa waumini na wadau wote kwa ushirikiano wao katika kujenga kanisa imara.Kwa ujumla, miaka mitano ya uongozi wa Askofu Dkt. Mbilu imeacha alama ya kudumu. Ni safari ya mageuzi, umoja na uthabiti wa Imani msingi imara kwa maendeleo ya sasa na ya vizazi vijavyo, uongozi wake unaoneka katika mambo yafutaoyo

Amefanikiwa kwa sehemu kubwa Kujenga na Kudumisha Umoja wa Kanisa: Moja ya mafanikio makubwa ya Askofu Dkt. Mbilu ni kuimarisha umoja ndani ya Dayosisi. Kupitia mikutano ya mara kwa mara ya Wachungaji, Wazee wa Kanisa na Waumini, pamoja na mafundisho yanayosisitiza upendo na mshikamano, amefanikiwa kupunguza migawanyiko iliyokuwa ikijitokeza hapo awali. Umoja huu umeonekana si tu katika Ibada bali pia katika ushirikiano wa miradi ya maendeleo na huduma za kijamii.

Dayosisi kuaminiwa na Serikali na Marafiki wa Maendeleo: Katika kipindi cha miaka mitano, Askofu Dkt. Mbilu amefanikiwa kurejesha imani ya Serikali na marafiki wa maendeleo ndani na nje ya nchi kwa dayosisi. Hii ni kutokana na uongozi wake kuweka mkazo katika uwazi wa matumizi ya rasilimali, uwajibikaji na usimamizi bora wa miradi. Hali hii imeifanya Dayosisi kuwa mshirika anayeaminika tena katika utekelezaji wa miradi ya kijamii kama vile Elimu, Afya na Diakonia.

Ushiriki katika kazi za umoja wa KKKT: Askofu Dkt. Mbilu ameonyesha mfano wa uongozi unaoshirikiana kwa karibu na ngazi za juu za KKKT. Amehakikisha Dayosisi yake inashiriki kikamilifu katika shughuli za kitaifa za kanisa, ikiwemo mikutano, semina na programu za maendeleo ya kiroho. Ushiriki huu umeongeza mchango wa Dayosisi katika maamuzi ya Kanisa zima na kuimarisha mshikamano wa kitaifa.

Kuboresha huduma za Diakonia: Huduma za diakonia zimepata msukumo mpya chini ya uongozi wake. Dayosisi imeongeza juhudi katika kusaidia makundi yenye uhitaji maalum, ikiwemo Yatima, Wajane na Watu wenye Ulemavu. Pia, kumekuwa na uwekezaji katika sekta za Afya na elimu, ambapo hospitali na shule zinazomilikiwa na kanisa zimeboreshwa kwa kiwango kikubwa.

Kuimarisha utawala bora na mipango endelevu: Mbali na maeneo yaliyotajwa, uongozi wake umejikita pia katika kuimarisha mifumo ya utawala bora ndani ya Dayosisi. Amehimiza matumizi ya mipango mkakati, tathmini ya mara kwa mara na uwekaji wa vipaumbele vinavyolenga maendeleo endelevu. hii imeifanya Dayosisi kuwa na mwelekeo ulio wazi na unaopimika.

Haya ni mafanikio yanayostahili pongezi kubwa kwa waumini wote, viongozi wa Kanisa katika ngazi mbalimbali, pamoja na washirika wa maendeleo walioungana kwa moyo wa kujitoa na uwajibikaji. ni ushuhuda kuwa kwa umoja na uongozi thabiti, changamoto kubwa zinaweza kushughulikiwa kwa mafanikio.

Katika kipindi hiki cha miaka mitano ya uongozi wa Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, licha ya kuikuta Dayosisi ikiwa katika changamoto kubwa za kiuchumi na kiutawala, mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta zote za huduma za jamii kama ifuatavyo:

Afya: Ukarabati wa miundombinu muhimu ya Afya ikiwemo kliniki ya Afya ya akili Korogwe, wodi ya wazazi Bumbuli na jengo la watoto wachanga (NICU).Ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa na mashine ya usingizi (jumla ya zaidi ya Mil. 88). Kuimarika kwa ushirikiano na Serikali (PPP) uliosaidia upatikanaji wa ruzuku na watumishi. Kuanzishwa kwa mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa fedha na huduma za Afya.Kupatikana kwa gari jipya Hospitali ya Afya ya Akili Lutindi.

Diakonia: Uboreshaji mkubwa wa vituo vya huduma za kijamii Irente (yatima, wasioona, na wenye ulemavu wa akili/usonji).Ujenzi wa bweni la kisasa kwa watoto wenye mahitaji maalum (gharama Mil. 172).Kuanzishwa kwa vituo 4 vya malezi ya watoto na vijana kwa kushirikiana na Compassion International.Uanzishaji wa miradi ya kiuchumi (nyuki, greenhouse, kilimo na ufugaji) kwa ajili ya kujitegemea.Kupatikana kwa usafiri (gari) katika kituo cha watoto yatima.

Elimu: Kuanzishwa kwa Taasisi ya Ufundi KOTETI yenye wanafunzi 151.Ongezeko kubwa la udahili wa wanafunzi katika shule za sekondari (mfano Lwandai kutoka 8 hadi 63) Kuimarika kwa ufaulu hadi kufikia matokeo ya kiwango cha juu (Division I yenye A zote).Ukarabati wa miundombinu ya shule na kurejeshwa kwa kituo cha mitihani. Kupatikana kwa ithibati (accreditation) ya KOTETI na kuandaliwa kwa mtaala/kitabu cha elimu maalumu. Kufanyika kwa warsha ya kitaifa ya elimu maalumu.

Idara ya Jinsia na Watoto: Kuanzishwa kwa kitengo cha wanaume na kuhamasisha ushiriki wao katika ujenzi na maendeleo ya Kanisa.Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sharika (madarasa, ofisi, vyoo, minara ya kengele n.k).Kuimarika kwa mradi wa wanawake (vitenge) uliokua kutoka mikopo ya Mil. 25 hadi mtaji wa Mil. 34.

Vijana na UKWATA: Kuimarika kwa mikutano ya UKWATA kila mwaka. Kufanyika kwa matamasha makubwa ya vijana (2023 & 2025) yaliyohusisha zaidi ya vijana 2,000.Kuimarisha malezi ya vijana kiroho, kiuchumi, kiafya na kijamii.

Kwa ujumla, uongozi wa Askofu Dkt. Mbilu umeleta mageuzi makubwa katika huduma za jamii ndani ya kipindi kifupi cha miaka mitano, ukiweka misingi imara ya maendeleo ya kiroho, kijamii na kiuchumi ya Dayosisi.

Katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Askofu Dkt. Mbilu, Kurugenzi ya Uchumi, Mipango na Maendeleo imefanikiwa kuleta maendeleo makubwa ya kiuchumi, kijamii na miundombinu ndani ya Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kupitia idara zake mbalimbali.

Maendeleo ya Kilimo, Ardhi na Misitu:Kuanzishwa kwa shamba la parachichi (ekari 30) Irente.

uzalishaji wa miche zaidi ya 45,000 ya miti (Irente na Soni). Upandaji wa miti zaidi ya 20,000 katika maeneo mbalimbali ya Dayosisi. Uanzishwaji wa ufugaji nyuki (mizinga 200) na uzalishaji wa zaidi ya lita 1,000 za asali kwa mwaka.

Kupunguza Umaskini na Uwezeshaji wa Jamii:Kutolewa kwa elimu ya kuweka na kukopa (SACCOS) katika sharika mbalimbali kwa ushirikiano na UEM.Kuanzishwa kwa SACCOS ya watumishi wa Dayosisi, inayochangia ustawi wa kiuchumi wa watumishi.Uboreshaji wa Miundombinu. Ujenzi wa vibanda 17 vya biashara katika eneo la ofisi kuu. Ukarabati wa ofisi kuu ikiwemo upakaji rangi na ujenzi wa choo cha kisasa.

Ukarabati wa vyumba 6 vya kisasa na ukumbi wa chakula Tumaini Hostel,Ujenzi wa chumba cha kisasa Irente Farm,Kuanzishwa kwa huduma mpya ya usambazaji wa maziwa ya mtindi, Kuendelezwa kwa shughuli za ufugaji wa nguruwe, Ukarabati wa Tumaini Mbuyukenda Hostel na Vuga Press (miundombinu na mashine), Kuanzishwa kwa huduma ya bima kupitia Zanzibar Insurance Corporation (ZIC) katika Bookshop ya Dayosisi.

Kwa ujumla, uongozi wa Askofu Dkt. Mbilu umeleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na maendeleo endelevu, kwa kuimarisha uzalishaji, kuongeza vyanzo vya mapato, kuboresha huduma na kuwezesha jamii kiuchumi ndani ya Dayosisi.

Mnamo tarehe 26/11/2020 Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alichaguliwa kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Askofu Dkt. Mbilu alichaguliwa kuwa Askofu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki baada ya kufanyika Mkutano Mkuu wa 3 baada ya miaka 125 ya Injili ulioanza tarehe 25-26/11/2020, mkutano uliokuwa na ajenda kuu moja ya Uchaguzi wa Askofu mpya wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na viongozi wengine.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati maalumu ya kuratibu shughuli za mkutano mkuu wa uchaguzi alikuwa Askofu Mstaafu Dkt. Paulo Akyoo toka KKKT Dayosisi ya Meru ambaye baada ya uchaguzi alimtangaza Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliye chaguliwa na Wajumbe wa mkutano Mkuu kuwa Askofu mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa kupata kura 194 sawa na 89.4% .

Askofu Mteule alimteua Mch. Michael Mlondakweli Kanju ambaye alithibitishwa na Mkutano Mkuu kwa kura ya Siri na kufanikiwa kupata kura 170 Kati ya 210 sawa na 80.9%. Kura hizo ni zaidi ya 2/3 ambalo ni hitaji la kikatiba. Aidha Mkutano Mkuu ulichagua wajumbe wa Halmashauri kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki. Baada ya kupatikana kwa

Halmashauri kuu hiyo ilitimiza wajibu wake wa Kikatiba wa kuchagua Wakuu wa Majimbo na kuwaleta mbele ya Mkutano mkuu.

Askofu Dkt. Mbilu ambaye alizaliwa tarehe 9 Mei, 1968 katika kijiji cha Kwang’wenda, Soni, Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga, alianza wajibu aliopewa kuiongoza KKKT-DKMs katika nafasi ya Uaskofu tarehe 09/05/2021, siku ambayo aliingizwa kazini kuwa Askofu wa 5 wa KKKT-DKMs.

Askofu Dkt. Mbilu alibarikiwa kuwa Mchungaji Februari 19, 1995, alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Kwang’wenda, Lushoto. Mwaka 1985-1988 alipata elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Namfua iliyopo Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro. Alipata elimu ya Theologia, Chuo cha Theologia, Makumira mwaka 1990- 1994 na kumaliza masomo ya General Certificate in Theology.

Mwaka 1997 alijiunga na masomo ya shahada ya Theolojia Chuo kikuu cha Makumira na kuhitimu mwaka 2000. Alipata shahada ya uzamili ya Theolojia mwaka 2000-2002 huko Norway, katika chuo cha Stavanger School of Mission and Theology.

Mwaka 2006-2012 alijiunga na chuo kikuu cha Kirchliche Hochschule Wuppertal cha nchini Ujerumani ambapo alitunukiwa shahada ya uzamivu katika Theolojia. Mwaka 1996 nilisoma Kozi Maalum ya Music Day Star University Nairobi Kenya (Church Music and African Traditional Music) amewahi pia kuwa Mwalimu katika Chuo cha Biblia Vuga 1994-1997 na pia amewahi kuwa Mchungaji Kiongozi Usharika wa Mombo, mwaka 1997-1999 na Usharika wa Korogwe 2003.

Aliwahi pia kuwa Mkuu wa Jimbo la Kaskazini na Mchungaji wa Usharika wa Mlalo kuanzia mwaka 2004 hadi 2006, na mwaka 2012 alikuwa Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kange. Askofu Dkt. Mbilu amewahi kuwa Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira 2012- 2015.

Mwaka 1996 nilisoma Kozi Maalum ya Music Day Star University Nairobi Kenya (Church Music and African Traditional Music)

Pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa kituo cha Tanga cha Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastiani Kolowa, (SEKOMU) mwaka 2015-2016. Vilevile alikuwa Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho kati ya mwaka 2016 hadi 2018 na mhadhiri chuoni hapo katika masomo ya Agano Jipya na Lugha za Biblia (Kigiriki).

Hadi siku anachaguliwa kuwa Askofu Mteule, Askofu Dkt. Mbilu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo kikuu cha Silliman kilichoko nchini Philippines, akifundisha masomo ya Agano Jipya na Lugha za Biblia (Greek na Hebrew).

NDOA

Alifunga ndoa na Dkt.Mary Joseph Jali Desemba 9, 1995 na wamejaliwa kupata watoto watatu, Dkt.Sarah Mbilu, Mhandisi Joseph Mbilu, na Jackson Mbilu.

Kwa ujumla, miaka mitano ya uongozi wa Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu imeacha alama ya kudumu katika KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki siri kubwa ya mafanikio haya ni uongozi wa Askofu Dkt. Mbilu uliokuwa shirikisha na kutambua mchango wa kila Mwanadayosisi na wadau wengine . Ni kipindi kilichojengwa juu ya mafanikio ya kuimarisha umoja, kurejesha imani ya wadau, kulinda mafundisho sahihi ya neno la Mungu na kuleta maendeleo ya kijamii. Uongozi wake umeweka msingi imara kwa siku zijazo za dayosisi na kanisa kwa ujumla.

Ukiangalia kazi zilizofanyika ndani ya miaka 5 iliyopita, unaweza kuona kwa uhalisia kabisa vipaumbele vinavyoweza kuongoza miaka 5 ijayo. Hivi hapa ni mambo 10 yenye mantiki na msingi wa moja kwa moja kutoka kwenye mafanikio yake

Kuimarisha mafundisho sahihi ya neno la Mungu (Theolojia) Kwa kuwa Askofu Dkt. Mbilu ni msomi wa theolojia ataendelea kulinda kanisa dhidi ya mafundisho potofu na kuimarisha elimu ya Biblia.

Kumaliza kabisa deni la Dayosisi: ameshalishusha kutoka bilioni 7.6 hadi 2.3 hatua inayofuata ni kulifuta kabisa hili litafungua nguvu ya uwekezaji kwenye huduma na miradi mipya kupanua miradi ya kiuchumi na kujitegemea,miradi ya nyuki, kilimo, hostel, na uzalishaji itaongezwa zaidi lengo: dayosisi ijitegemee kifedha bila kutegemea wafadhili kwa sehemu kubwa.

Kuimarisha zaidi huduma za Afya baada ya maboresho ya hospitali na vifaa tiba kipaumbele kitakuwa kupanua huduma (specialized care, digital health).

Kukuza ubora wa elimu na taasisi za Kanisa:KOTETI, shule za sekondari, na elimu maalum tayari zimeanza kuimarika hatua inayofuata ni kuongeza ubora wa kitaifa na kimataifa.

Kuendeleza uwezeshaji wa vijana (ajira + uongozi) hapa miaka ijayo itaweka mkazo kwenye ajira kwa vijana Ubunifu wa kidigitali Uongozi wa kizazi kipya.

Kuimarisha teknolojia na mifumo ya kisasa tayari ameanzisha mifumo ya kielektroniki kwenye afya na fedha. Miaka ijayo inaweza kuona: Kanisa la kidigitali, Usimamizi wa kisasa wa data na huduma za mtandaoni.

Kuongeza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa amefanikiwa kurejesha imani ya serikali na wafadhili. hatua inayofuata: kupanua partnerships kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi.Kuimarisha umoja wa Kanisa na uongozi shirikishi hili ndilo msingi wa mafanikio yote aliyopata. Ataendelea kuzuia migawanyiko kuimarisha mawasiliano kujengauongozi wenye uwajibikaji.

Kwa kifupi, miaka 5 ijayo ya uongozi wake itaonekana kama awamu ya pili ya mageuzi: Kutoka “kujenga msingi” kwenda ubora wa juu