Contact Info

P.O Box 10 Lushoto Tanga Tanzania

+255

headoffice@elctned.org

ELCTNED

Latest Posts

Utiaji saini mkataba wa mradi mpya wa kuimarisha Afya na Makuzi ya watoto wadogo

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph. Mbilu leo tarehe 28/09/2026 amekutana na Wahadhiri Kutoka Chuo Kikuu cha Leibniz Hannover Ujerumani,Meike Albrecht na Kirsten Anna Beta katika hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa mradi mpya wa kuimarisha Afya na Makuzi ya watoto wadogo, hususani Watoto Yatima na walio kwenye Mazingira hatarishi (A Network of Knowledge: Fostering Early Childhood Health in Low-resource Communities – Prevention and Education through a Community-Based Network in Rural Tanzania).


Lengo la Mradi huu ni kuwajengea Maarifa ya kuimarisha Afya na Makuzi ya Watoto Yatima na walioko kwenye Mazingira hatarishi Wafanyakazi wa Kituo cha Watoto Yatima Irente na Shule ya Watoto wenye Ulemavu wa Akili na Usonji Irente (Irente Rainbow School), pamoja na jamii kwa ujumla ili kuepusha Ulemavu na changamoto mbalimbali zinazoweza kuwaathiri Watoto walio kwenye makundi haya. Mradi huu ni wa miaka mitatu na unatarajiwa kufanyika kwenye Vituo hivyo na kwenye Majimbo 5 ya Dayosisi ambayo yapo katika Mkoa wote wa Tanga.

Pamoja na mafunzo yatakayotolewa katika makundi hayo, Mradi huu una lengo la kuimarisha kozi mpya ya Elimu ya Awali na Makuzi (Early Childhood Education and Development) itakayoanzishwa katika Taasisi ya Elimu ya KOTETI.Mradi huu unafadhiliwa na Wizara ya Mambo ya Jamii, Afya na Usawa- Jimbo la Lower Saxony Ujerumani.