Contact Info

P.O Box 10 Lushoto Tanga Tanzania

+255

headoffice@elctned.org

ELCTNED

Latest Posts

Ziara ya kikazi ya Askofu Dkt. Mbilu nchini Ujerumani yaendelea kuzaa matunda

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu anaendelea na ziara yake ya kikazi nchini Ujerumani kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Dayosisi na washirika wake wa maendeleo pamoja na makanisa rafiki.

Mnamo tarehe 15 Juni, Baba Askofu alitembelea ofisi za United Evangelical Mission (UEM) mjini Wuppertal, ambapo alitoa taarifa kuhusu maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na UEM. Miongoni mwa miradi hiyo ni ule wa uimarishaji wa Shamba la Irente pamoja na miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa katika Dayosisi.

Katika siku hiyo hiyo, Baba Askofu alipata fursa ya kufanya kikao muhimu na Dr. Thorsten Latzel, Mkuu wa Evangelical Church in the Rhineland. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Dr. Wibke Janssen pamoja na Joachim Deterding.Katika mazungumzo hayo, Baba Askofu alieleza kwa uwazi changamoto ya deni linaloikabili Dayosisi na namna lilivyoathiri utekelezaji wa kazi za Diakonia na Injili. Alibainisha kuwa licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na uongozi wa Dayosisi, sehemu kubwa ya rasilimali imeelekezwa katika ulipaji wa deni hilo, hali iliyosababisha baadhi ya shughuli za huduma na uinjilisti kusuasua.Kwa upande wake, Dkt. Latzel alionesha utayari na moyo wa kuunga mkono juhudi za Dayosisi katika kukabiliana na changamoto hizo. Ingawa hakutaja kiwango cha msaada kitakachotolewa, alisisitiza nia yake ya kutafuta namna ya kusaidia baada ya kukamilisha mashauriano na vikao vya maamuzi vya kanisa lake.

Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Kirchliche Hochschule Wuppertal. Baba Askofu aliambatana na Katibu Mkuu wa Dayosisi, Mwl. Julius Madiga, pamoja na Mama Askofu Dkt. Mary Mbilu na kijana wao, Mhandisi Joseph Mbilu.Aidha, Baba Askofu alitembelea Usharika wa Holten-Sterkrade uliopo Jimbo la Oberhausen, ambao una ushirikiano wa karibu na Usharika wa Magamba.

Ziara hiyo ililenga kuimarisha zaidi mahusiano yaliyopo kati ya sharika hizo. Usharika wa Holten-Sterkrade umekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia ujenzi wa Kindergarten ya Usharika wa Magamba.

Wakati wa ziara hiyo, Baba Askofu pia alipata nafasi ya kukutana na Kamati ya Undugu ya Jimbo la Oberhausen, ambalo lina uhusiano wa muda mrefu na Jimbo la Kusini. Kupitia mikutano hiyo, aliwashirikisha marafiki na wadau wa maendeleo kuhusu kazi mbalimbali zinazotekelezwa na Dayosisi, mafanikio yaliyopatikana katika miradi ya maendeleo ikiwemo kilimo cha parachichi, maduka ya biashara na shughuli nyingine za kiuchumi.

Kwa ujumla, ziara hiyo imekuwa na mafanikio makubwa katika kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya majimbo, sharika na vituo mbalimbali. Vilevile, imekuwa fursa muhimu ya kueleza mafanikio, changamoto na mikakati ya Dayosisi katika kuendelea kutekeleza huduma ya Injili na maendeleo kwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*