Tarehe 6/11/2026 Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Burian, kwa ajili ya kikao cha tathmini ya michango ya Harambee iliyozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, tarehe 5/10/2026.
Katika kikao hiki ambacho Baba Askofu aliambatana na Mkuu wa Jimbo la Pwani Mch. Issai Mweta, Mkuu wa Mkoa alisisitiza umuhimu wa kuwafuatilia wale wote walioalikwa kwenye Harambee hii na walioahidi kutoa michango ili wakamilishe michango yao.
Aidha, wale ambao hawakufika amesisitiza wafuatiliwe ili, kupitia michango yao, taarifa kamili ya Harambee hii iweze kutumwa kwa Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Waziri Mkuu.Itakumbukwa kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, kwa kushirikiana na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, inayotoa huduma zake katika Mkoa mzima wa Tanga, waliandaa Harambee hii kwa ajili ya kuboresha kazi za vituo vya Dayosisi vinavyotoa huduma za jamii.
Miongoni mwa huduma za Dayosisi zinazogusa jamii kwa ujumla ni pamoja na Elimu, Afya, Maji na Diakonia, katika vituo vya Lutindi Mental Hospital, Bumbuli Lutheran Hospital, Kilindi Hospital, Kituo cha Watoto Yatima Irente, Shule ya Wasioona Irente, Shule ya Watoto Wenye Ulemavu wa Akili na Usonji (Irente Rainbow), Shule za Sekondari pamoja na Vyuo vya Kati.
Akaunti zetu zinazopokea Michango ya Harambee hii ni hizi zifuatazo:
A. Bank: NMB
Jina: ELCT NED HARAMBEE KUU ACCOUNT
Acc. No. 41610058009
Branch: Lushoto
B. Bank: CRDBJina: ELCT NED HARAMBEE KUU ACCOUNT
Acc.No.10457136884
Branch: Lushoto
Tufuatilie kupitia mitandao yetu rasmi:
Facebook Account: North Eastern Diocese Facebook
Page: ELCT – North Eastern Diocese YouTube: KKKT DKMS Online TV
Tovuti: www.elctned.org
+255743399798



