Contact Info

P.O Box 10 Lushoto Tanga Tanzania

+255

headoffice@elctned.org

ELCTNED

Latest Posts

Bw. Brian Gustafson kutoka Marekani afanya mazungumzo na Askofu Dkt. Mbilu

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 29 Septemba 2026 amekutana na Bw. Brian Gustafson kutoka Marekani, na kufnaya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Lushoto.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Bw. Gustafson na Dayosisi, pamoja na kujadili fursa mbalimbali za maendeleo zinazoweza kusaidia kuimarisha huduma na shughuli za Dayosisi.

Katika mazungumzo hayo, walijadili masuala mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo kuimarisha, kuweka mipango ya uboreshaji pamoja na kuanzisha mradi wa mazao yamisitu.

Mradi huo unatarajiwa kuwa sehemu ya juhudi za kuendeleza shughuli za kiuchumi na kimazingira, sambamba na kuchangia katika maendeleo endelevu ya Dayosisi.Bw. Brian Gustafson alifuatana na mkewe, Bi. Judy Gustafson, pamoja na mwenyeji wao Dkt. Philemon Mtoi.

Mazungumzo hayo ni ishara na hatua muhimu katika kuendelea kujenga na kuimarisha mahusiano ya ushirikiano kwa lengo la kushirikiana katika kutafuta fursa na mipango yenye manufaa kwa maendeleo ya Dayosisi na jamii kwa ujumla.