Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amefika kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mheshimiwa Balozi Dkt. Batilda Buriani kwa ajili ya kikao maalum cha maandalizi ya Harambee ya kuchangia kazi za Maendeleo ya Dayosisi na uboreshaji wa Vituo vya Huduma na Diakonia.
Katika Kikao hiki kilichofanyika leo tarehe 01/10/2026 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, pamoja na mambo mengine viongozi hawa wameangalia kwa mapana maandalizi mazima ya Harambee hii ikiwa ni pamoja na kupitia orodha ya Wageni walioalikwa, ratiba ya Harambee na majukumu ya makundi na watu mbalimbali.
Katika Kikao hiki Mkuu wa Mkoa ameungana na Mhandisi Emigidius Kasunzu, Katibu Tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji (kushoto kwa Mkuu wa Mkoa) ambapo Askofu Dkt. Mbilu aliambatana na Mkuu wa Jimbo la Pwani,-Tanga, Mch. Isai Mweta.
Mgeni Rasmi wa Harambee hii atakuwa Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Harambee hiyo itafanyika siku ya Jumatatu tarehe 05.10.2026 kuanzia saa 2:00 asubuhi na Waalikwa wote wanatakiwa kuwasili Tanga Beach Resort saa 1:00 Asubuhi.



