Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ametoapongezi kwa Mch Dkt. Godfrey Tahona Walalaze ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Mission na Uinjilisti KKKT kwa kuhitimu masomo yake ya Shahada ya Uzamivu (PhD) katikaTheolojia kutoka Chuo Kikuu cha South African Theological Seminary (SATS).
Mch. Dkt. Walalaze amefanya utafiti kuhusu Athari ya Athari ya matumizi ya lugha za Kidini katika Kampeni za Uchaguzi wa Rais nchini Tanzania kati ya mwaka 1995 na2020” (Analysis on Influence of Religious Rhetoric on Presidential Election Campaigns in Tanzania between 1995–2020).
Utafiti huu unapendekeza hatua za kisera kwa taasisi za uchaguzi, zikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), pamoja na maafisa wanaohusika na usimamizi wa kampeni.
Mapendekezo haya yanawapa wasimamizi wa uchaguzi na watunga sheria msingi wa kuweka kanuni zilizo wazi zaidi kuhusu matumizi ya lugha ya kidini katika kampeni za uchaguzi. Vilevile, utafiti unaweka msingi wa elimu ya uraia na elimu ya mpiga kura, na kutoa maarifa yanayoweza kusaidia kuongoza chaguzi zijazo.
Utafiti unaangazia jinsi matumizi ya lugha za kidini yanavyoweza kuwashawishi wapiga kura kwa mwelekeo chanya na ama hasi katika chaguzi za Tanzania, inakuza uelewa wa kinadharia, inawawezesha wananchi kuwa na uelewa mpana zaidi, inatoa taarifa muhimu kwa ajili ya uundaji wa kanuni za uchaguzi, na kulitaka Kanisa kuwa na msimamo ulio wazi wa kimaadili.
Utafiti unatoa tahadhari dhidi ya matumizi mabaya ya mamlaka ya kidini na kusisitiza matumizi yenye uwajibikaji ya ushawishi wa kidini ili kuimarisha ushiriki wa wananchi ulio na taarifa sahihi, maadili na tija.
Askofu Mbilu amesema kuwa ana mshukuru Mungu kuwa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ya KKKT imeongezewa idadi ya wasomi wabobezi wa maswala mbalimbali.
Akieleza furaha yake Askofu Dkt. Msafiri Mbilu, ameeleza kuwa katika kipindi hiki Mungu amefungua milango kwa Wachungaji na Wana Dayosisi wengine kujiendeleza na kupata Shahada za Udaktari jambo ambalo ni fahari kubwa sana kwa Dayosisi. Pamoja na Dkt. Walalaze wengine waliomaliza masomo yao hivi karibuni ni pamoja na:
Mch. Dkt. Nuru Mwakapusya
Mch. Dkt. Lemi BarutiMwl.
Dkt. Mary Joseph Jally
Dkt. Christopher Mdoe
Dkt. Philemon Mtoi
Hawa wote wanaleta heshima kubwa kwa Dayosisi yetu.nawahimiza vijana wengine kuendelea kusoma na kufanya tafiti mbalimbali zitakazoleta tija kwa Dayosisi na Taifa. Vijana wasijiingize sana katika kutegemea Digree za kupewa bila kufanya tafiti kwa kuwa ulimwengu wa sasa unahitaji watafiti ili kuleta mchango katika kutatua changamoto mbalimbali" Alisema Askofu Dkt. Msafiri Mbilu.
Mch. Dkt. Nuru Mwakapusya amehitimu Shahada ya Uzamivu ya Theolojia yaani (Doctor of Theology) akiwa amebobea katika Maadili ya Kikristo (Christian Ethics). Alianza masomo yake mwaka 2022 na kuhitimu mwaka 2026.
Katika utafiti wake wa shahada ya uzamivu uliokuwa na kichwa cha habari, "An Ethical Analysis of Church's Response to the Trafficking of Women in Tanga, Tanzania," Mch. Dkt. Nuru alichambua kwa kina mwitikio wa Kanisa katika kukabiliana na tatizo la usafirishaji haramu wa wanawake kwa mtazamo wa maadili ya Kikristo.
Matokeo ya utafiti huo yatalisaidia Kanisa na jamii kushirikiana katika kuelimisha waumini na wananchi kwa ujumla kuhusu madhara ya biashara haramu ya binadamu, kuhimiza ulinzi wa utu na haki za binadamu pamoja na kuimarisha huduma kwa waathirika.
Aidha, utafiti huo unahamasisha ushirikiano kati ya Kanisa, Serikali na wadau mbalimbali katika kuzuia biashara haramu ya binadamu na kujenga jamii yenye usalama, haki na heshima kwa wanawake na wasichana.
Mchungaji Dkt. Lemmi Tamilwai Baruti: amehitimu masomo ya Shahada ya Uzamivu (Doctor of Philosophy in Theology Systematic Theology) katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (University of South Africa – UNISA), kwa kipindi cha mwaka 2023 hadi 2026.
Utafiti wake unalenga kuchunguza nafasi ya Kanisa katika kuhamasisha maendeleo ya viwanda, kupunguza umasikini, kutetea haki za kiuchumi na kijamii, pamoja na kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa kuangazia masuala haya, utafiti wake unaweka msingi wa kutafakari namna mafundisho ya Kikristo na misingi ya kitheolojia inavyoweza kuhusishwa na changamoto halisi za kiuchumi na kijamii zinazolikabili taifa, hususani katika juhudi za kujenga uchumi unaozingatia haki, usawa na utu wa binadamu.
Utafiti huu unatoa mchango muhimu katika eneo la theolojia ya kimfumo, haki za binadamu, haki ya kijamii na heshima ya utu wa binadamu.
Aidha, mfumo unaopendekezwa katika utafiti huo unatoa mtazamo wa namna maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanavyoweza kuimarishwa kupitia ushirikiano wenye tija kati ya Kanisa na Serikali. Ushirikiano huo unalenga kuchochea mabadiliko yanayoweza kuleta manufaa kwa wananchi, hasa katika masuala ya uzalishaji, kupunguza umasikini na kuboresha ustawi wa jamii.
Utafiti huu pia unaibua nafasi ya Kanisa katika kushiriki mijadala ya kitaifa kuhusu sera za maendeleo, kwa kuzingatia misingi ya imani, haki, uwajibikaji na huduma kwa jamii.
Dkt. Mary Joseph Jally
Shahada: Doctor of Education (Ed.D.)
Taaluma Kuu (Major): Educational Management
Chuo: Negros Oriental State University
Kampasi Kuu: Dumaguete City
Nchi: Philippines
Taarifa za Utafiti Mada ya Utafiti (Research Title):Assessing Teaching Competence Across Grade 3 to 7 Teachers of the Republic of Tanzania, East Africa.
Eneo la Utafiti: Uwezo na Umahiri wa Ufundishaji wa Walimu katika Shule za Msingi (Teaching Competence of Teachers in Primary Schools).
Utafiti huu wa Dkt. Mary Jally una umuhimu mkubwa kwa jamii na Kanisa kwa ujumla. Kwanza, ni muhimu kwa jamii tuliyonayo kuifahamu hali halisi ya jamii ya sasa, pamoja na kutambua mchango wa mwalimu katika kujenga Taifa bora, imara na thabiti.
Kupitia ujuzi, uwezo na umahiri (Competence) wa kila mwalimu mmoja mmoja, tunaweza kujenga kizazi bora, chenye uwezo wa kukabiliana na changamoto mbalimbali na kilicho imara katika maisha (Stahimilivu).Vilevile, utafiti huu una umuhimu kwa Kanisa kwa ujumla, kwa kuwa elimu na umahiri wa walimu vina mchango katika malezi, makuzi na maendeleo ya jamii. Hivyo, kuelewa uwezo na umahiri wa walimu ni hatua muhimu katika kuimarisha elimu na kujenga jamii bora kwa manufaa ya Taifa na Kanisa.
Dkt. Christopher N. Mdoe (PhD)Shahada ya Uzamivu (PhD) amehitimu Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Sera, Mipango na Usimamizi (Policy, Planning and Management) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sokoine University of Agriculture – SUA), Morogoro, Tanzania. Alianza masomo ya Shahada ya Uzamivu mwezi Machi 2023 na kukamilisha utafiti wake mwezi Machi 2025, ndani ya kipindi cha miaka miwili tangu kuanza masomo hayo, na kutunukiwa shahada hiyo mwezi Oktoba 2025.
Alisoma katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kilichopo Morogoro, Tanzania, chini ya Idara ya Sera, Mipango na Usimamizi (Department of Policy, Planning and Management), katika Kitivo cha Sayansi za Jamii (College of Social Sciences and Humanities).Utafiti : (“Implications of Climate-Smart Aquaculture Practices on Households’ Well-Being in Lake Zone Regions of Tanzania”), yaani, Mchango wa Mbinu za Ufugaji wa Samaki Zinazoendana na Mabadiliko ya Tabianchi katika Ustawi wa Kaya katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa Tanzania.Utafiti huu ulichunguza namna mbinu za ufugaji wa samaki zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi zinavyoweza kuchangia kuboresha ustawi wa kaya zinazojishughulisha na ufugaji wa samaki, hususani kuongeza kipato cha kaya na kuboresha usalama wa chakula.
Kwa namna mahususi, utafiti ulichunguza mbinu mbalimbali za ufugaji wa samaki zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi, kutathmini maeneo yanayofaa kwa shughuli hizo kwa kutumia taarifa za kijiografia, kuchambua mambo yanayoathiri matumizi ya mbinu hizo, na kutathmini uhusiano wake na kipato cha kaya pamoja na usalama wa chakula. Utafiti ulifanyika katika mikoa ya Mwanza na Mara.
Mchango wa Utafiti kwa Kanisa na jamii?Utafiti huu unatoa maarifa na ushahidi wa kitaalamu unaoweza kusaidia Kanisa na jamii katika kuendeleza shughuli za kujipatia kipato kwa njia endelevu, kuimarisha usalama wa chakula, kuhifadhi mazingira na kuwawezesha wananchi kiuchumi.Kwa upande wa Kanisa, matokeo ya utafiti yanaweza kutoa fursa za kubuni na kuendeleza miradi endelevu ya kiuchumi itakayowanufaisha waumini na jamii zinazolizunguka Kanisa. Maarifa haya yanaweza kutumika katika kuanzisha na kuimarisha miradi ya kijamii inayohusisha ufugaji wa samaki, kilimo shirikishi, uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Jitihada hizo zinaweza kuunga mkono utume wa Kanisa wa kuwahudumia watu na kuboresha ustawi wao.Kwa upande wa jamii, utafiti unaonesha fursa za kuongeza kipato cha kaya, kuboresha upatikanaji wa chakula chenye lishe bora, kuimarisha uwezo wa wananchi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali za asili.
Aidha, unasisitiza umuhimu wa kuboresha upatikanaji wa mikopo nafuu, huduma za ugani, teknolojia zinazofaa na mafunzo, hususan kwa wanawake na vijana.Dkt. Christopher N. Mdoe anatoa shukrani kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT–DKMs), hususani Baba Askofu, Dkt. Msafiri J. Mbilu, kwa maombi yake, mwongozo wa kiroho, maneno ya kutia moyo na ushirikiano wake katika kipindi chote cha masomo yake. Maneno yake ya kutia moyo na namna alivyoendelea kunitia nguvu katika safari hii vimekuwa chachu kubwa ya kunipa moyo na uvumilivu.
Vilevile, ninawashukuru sana Wachungaji, Wahudumu wa Kanisa na Wakristo wote wa Dayosisi ambao waliniombea, kunitia moyo na kunisaidia kwa namna mbalimbali. Mchango wao wa kiroho umekuwa wa thamani kubwa katika kufanikisha safari hii.Alisema Dkt. Christopher MdoeAidha, ametoa shukrani za dhati kwa wazazi wake, Mwl. Stephen Mdoe na Bi. Rachel Mdoe,pamoja na familia yake kwa ujumla, kwa upendo wao usio na kipimo, uvumilivu, maombi, uelewa na moyo wa kumtia moyo katika kipindi chote cha masomo yake.
Msaada wao, kujitoa kwao na kunitia moyo mara kwa mara vilinipa nguvu na azma ya kuvumilia hadi kufikia mafanikio haya. Pia, ninatoa shukrani za pekee kwa walimu wangu wote, kuanzia ngazi ya elimu ya msingi na katika hatua zote za safari yangu ya elimu, kwa kujitoa kwao, juhudi na mchango wao mkubwa katika kujenga msingi imara wa elimu yangu ulionisaidia kufikia hatua hii. Shukrani zangu za dhati pia ziwaendee wasimamizi wangu wa kitaaluma katika utafiiti wangu Prof Christopher Mahonge na Prof Edwin Ngowi kwa mwongozo, ushauri, malezi ya kitaaluma na msaada wao katika kipindi chote cha utafiti, pamoja na watu wote walioshiriki kwa namna mbalimbali kufanikisha masomo yangu. Aliongeza Dkt. Mdoe.
Dkt. Philemon Mtoi, amehitimu kwa mafanikio na kiwango cha juu cha usomi cha Doctor of Philosophy (Ph.D.) in History, akijikita hasa katika Historia ya Tiba na Magonjwa (History of Medicine and Disease) pamoja na Historia ya Ukoloni. Alitetea tasnifu yake (Thesis Defense) kwa mafanikio mnamo Machi 10, 2026. Alianza rasmi masomo yake ya PhD mnamo mwaka April 2022 na kukamilisha mapema mwaka 2026.
Masomo yake ya Udaktari wa Falsafa aliyasomea katika Chuo Kikuu cha Bonn (The University of Bonn) nchini Ujerumani. Kabla ya hapo, alipata Shahada ya Uzamili (Master of Arts in History) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Utafiti wake wa PhD ulijikita kwenye mada isemayo: "The interface between German health policies and indigenous health systems in Northeastern Tanzania from 1884 to 1914".Katika utafiti alichunguza mwingiliano, migongano, na ushirikiano kati ya sera za afya za utawala wa kikoloni wa Kijerumani na mifumo ya afya ya asili (tiba za kienyeji) ya wenyeji wa Kaskazini-Mashariki mwa Tanzania (hususan maeneo ya Usambaa/Lushoto) wakati wa ukoloni.
Utafiti wake una umuhimu mkubwa katika ukombozi wa kifikra (decolonization) kwa kuandika historia ya Afrika kupitia mtazamo wa Kiafrika. Unasaidia jamii kutambua na kuthamini mifumo yao ya asili ya afya na jinsi jamii hizo zilivyokuwa na uwezo wa kuhimili magonjwa na majanga kabla na wakati wa kuingiliwa na mifumo ya kigeni.
Umuhimu wa utafiti wake katika Kanisa kwa kuwa maeneo mengi ya Kaskazini-Mashariki mwa Tanzania (kama Lushoto) yalianzishwa vituo vya misheni ya Kikristo (kama vile Walutheri), utafiti huu unasaidia Kanisa kuelewa kihistoria jinsi taasisi za kidini zilivyoshirikiana au kuingiliana na mifumo ya wenyeji katika kutoa huduma za afya. Unalipa Kanisa mwongozo wa jinsi ya kuendeleza huduma za kijamii na kiroho kwa kuheshimu utamaduni na ustahimilivu wa jamii husika.



