Contact Info

P.O Box 10 Lushoto Tanga Tanzania

+255

headoffice@elctned.org

ELCTNED

Latest Posts

Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Korogwe, Jimbo la Tambarare

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, leo tarehe 15/11/2026 ameongoza Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Korogwe, Jimbo la Tambarare.Kabla ya kuanza kwa ibada hiyo, kulifanyika ibada ya uwekaji wakfu wa gari jipya aina ya Toyota Land Cruiser Hard Top, lililonunuliwa kwa ajili ya Jimbo la Magharibi. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Dayosisi za kuimarisha huduma na shughuli za Kanisa katika majimbo yake.

Ununuzi wa gari hilo ulitokana na maamuzi ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kilichofanyika tarehe 23–24 Aprili 2026, Utondolo, Lushoto. Kupitia Agenda Na. 5 iliyohusu mambo kutoka Kamati ya Utendaji, kikao hicho kiliazimia ununuzi wa gari hilo kwa ajili ya Jimbo la Magharibi.Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesema ni jambo la kumshukuru Mungu kuwawezesha wana Dayosisi kufanikisha upatikanaji wa gari hilo kupitia fedha za ndani za Dayosisi.

Alieleza kuwa hatua hiyo ni ushahidi wa juhudi za pamoja katika kuimarisha uwezo wa kiutendaji na kurahisisha utekelezaji wa shughuli na huduma za Kanisa.Katika ibada hiyo, Usharika wa Korogwe pia ulipokea Tuzo ya Pongezi kwa kuchangia Deni la Dayosisi, baada ya kufanikisha uchangiaji wa jumla ya Tsh. 257,532,000.Uongozi wa Dayosisi ulitoa shukrani za dhati na pongezi kwa washiriki wote wa Usharika wa Korogwe kwa kukamilisha kiwango chao cha uchangiaji wa deni hilo.

Usharika huo umefanikiwa kushika nafasi ya 15 kati ya sharika 76 za Dayosisi katika kutimiza lengo la uchangiaji kwa wakati.Aidha, katika ibada hiyo, jumla ya wanafunzi 89 wa Kipaimara walibarikiwa na 5 kati yao walibatizwa.“Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.” (Kutoka 33:14)