Contact Info

P.O Box 10 Lushoto Tanga Tanzania

+255

headoffice@elctned.org

ELCTNED

Latest Posts

Ziara ya Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu Bungeni Dodoma

Dodoma, 31 Agosti 2026 — Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) Tanga, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 31 Agosti 2026 yupo Bungeni Dodoma katika ziara maalum yenye lengo la kushirikisha na kuwaalika viongozi pamoja na wadau mbalimbali kushiriki katika Harambee ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, inayolenga kuchangia na kuboresha Vituo vya Huduma na Diakonia katika Dayosisi.Katika ziara hiyo, Askofu Dkt. Mbilu amekutana na Wabunge wote wa Mkoa wa Tanga, ambao wamepokea kwa uzito mkubwa wito na mpango huo wa Dayosisi. Wabunge hao wameonesha utayari wa kutoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha Harambee hiyo, wakitambua umuhimu wa kuboresha huduma za kijamii na kiroho zinazotolewa kupitia Vituo vya Huduma na Diakonia.
Aidha, katika ziara hiyo , Askofu Dkt. Mbilu amepata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali, akiwemo , Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mussa Zungu, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mheshimiwa Mary Chatanda, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Awesso, pamoja na Waziri wa ElimuMheshimiwa Prof. Adolf Mkenda.
Harambee hiyo ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki inatarajiwa kufanyika tarehe 20 Septemba 2026, Jijini Tanga, ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unawakaribisha waumini, Wanadayosisi, taasisi, viongozi, wafanyabiashara, wadau wa maendeleo na watu wote kuungana pamoja katika kufanikisha Harambee hii muhimu. Ushiriki wa kila mmoja, kwa namna yoyote ile, utakuwa sehemu ya kujenga na kuimarisha Vituo vya Huduma na Diakoni ili viweze kutoa huduma bora, zenye tija na zinazogusa mahitaji ya jamii.

Tufuatilie/Wasiliana nasi.
INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV
WEBSITE: www.elctned.org
Email: harambee@elctned.org
SIMU: 0743 399 798
BANK NMB
Jina: ELCT NED HARAMBEE KUU ACCOUNT
Acc.No. 41610058009,
Branch: Lushoto
BANK: CRDB
Jina: ELCT NED HARAMBEE KUU ACCOUNT
Acc No: 10457136884
Branch: Lushoto