Contact Info

P.O Box 10 Lushoto Tanga Tanzania

+255

headoffice@elctned.org

ELCTNED

Latest Posts

KKKT Marathon 2026. Kimbia kwa moyo, saidia kwa upendo.

Mkuu wa KKKT, Askofu Dkt. Alex Malasusa, amemkabidhi Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa Dayosisi ya KKKT Kaskazini Mashariki (DKMs) cheti cha ushiriki wa Dayosisi hiyo katika KKKT Marathon 2026, iliyofanyika leo tarehe 20 Juni 2026 jijini Arusha.

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliambatana na baadhi ya waumini wa Dayosisi ya KKKT-DKMs pamoja na viongozi mbalimbali wa Dayosisi hiyo katika kushiriki tukio hilo.

KKKT Marathon, ambayo hufanyika kila mwaka, mwaka huu imeongozwa na kaulimbiu isemayo: “Kimbia kwa Moyo, Saidia kwa Upendo.”Tukio hilo limeendelea kuhamasisha mshikamano, afya bora na moyo wa kusaidia wenye uhitaji kupitia ushiriki wa waumini na wadau mbalimbali.