Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, tarehe 13 Juni 2026 alishiriki Mkutano wa NED Roundtable uliofanyika Bethel nchini Ujerumani.
Mkutano huo uliwakutanisha marafiki na wadau mbalimbali wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kutoka maeneo tofauti ya Ujerumani.Miongoni mwa washiriki walikuwapo marafiki kutoka Majimbo ya Minden, Vlotho na Bielefeld pamoja na Kituo cha Bethel.
Aidha, mkutano huo ulihudhuriwa na Dr. Albrecht Philipps, Mkuu wa Masuala ya Misioni na Ekumene wa Kanisa la Westphalia.Vilevile, marafiki wa Shule ya Sekondari Lwandai kutoka Heinberg Gymnasium walishiriki mkutano huo huku, wakionesha nia ya kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo.
Mkutano huo ulikuwa fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuendeleza huduma na miradi inayounganisha Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na marafiki wake wa Ujerumani.



