Mnamo tarehe 10 Juni, Baba Askofu Dkt. Mbilu, amabaye akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini Ujerumani alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Jimbo la Minden, Bw. Michael Mertins.
Katika mazungumzo yao pamoja na mambo mengine , walijadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Jimbo la Kaskazini na wadau mbalimbali wa maendeleo nchini Ujerumani, kwa lengo la kuendeleza huduma za Kanisa kwa jamii.
Mazungumzo hayo yalijikita katika miradi mbalimbali ya kijamii inayogusa maisha ya watu moja kwa moja, hususani miradi ya maji safi na salama, ambayo ni sehemu ya huduma ya Kanisa katika kuboresha ustawi wa wananchi na kudhihirisha upendo wa Kristo kwa vitendo.
Ziara hii ina umuhimu mkubwa kwa Dayosisi kwani inaendelea kufungua milango ya ushirikiano wa kimataifa unaosaidia kuimarisha utume wa Kanisa katika nyanja za maendeleo ya kijamii, kiroho na kiuchumi. Kupitia mahusiano haya, Kanisa linaendelea kuwa chombo cha matumaini na maendeleo kwa waumini wake na jamii kwa ujumla.
Aidha, Mkuu wa Jimbo la Minden, Bw. Michael Mertins, lenye urafiki na Jimbo la Kaskazini, anatarajiwa kutembelea Dayosisis yetu hususani Jimbo la Kaskazini mwezi Agosti mwaka huu akiwa na msafara wa watu saba.
Ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo, kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali na kutafuta fursa mpya za kuendeleza huduma za Kanisa na maendeleo ya jamii.
Katika ziara hii Baba Askofu ameambatana na Katibu Mkuu Mwl. Julias Samwel Madiga pamoja na Mama Askofu, Dkt. Mary Mbilu.
Tunaendelea kumshukuru Mungu kwa kuongoza ziara hii ya Baba Askofu Dkt. Mbilu na kwa neema ya mahusiano mema yanayojengwa kwa ajili ya kuendeleza utume wa Kanisa na kuwahudumia watu wake.



