
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania Dkt. Fredrick Shoo amewataka waumini kujiepusha na mafundisho potofu ya neno la Mungu ambayo yamejitokeza hivi sasa ulimwenguni yenye kuyumbisha imani za waumini walio wengi.
Askofu Dkt. Shoo ameyasema hayo leo tarehe 28/07/2022 katika mwendelezo wa ziara yake anayoifanya ndani ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kuzungukia sharika mama,vituo mbalimba pamoja na kufungua na kuweka mawe ya msingi.Aidha amewataka waumini kutimilika katika Kristo ili kuweza kujiepusha na mafundisho hayo potofu .

Askofu Dkt. Fredrick Shoo akipanda mti akiwa katika Chuo cha Afya na Sayansi na Shirikishi Bumbuli
Sambamba na hayo Askofu Dkt. Shoo amechangia kiasi cha shilingi laki tano 500,000 kwaajili ya ujenzi wa Kanisa jipya linalojengwa katika Usaharika huo wa Bumbuli huku akitoa wito wa kutunzwa kwa Makanisa ya zamani yaliyojengwa na Wamisionari ili kuwa kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ametoa shukrani kwa Askofu Dkt. Shoo kwa kuendelea kusisitiza kuhusu umoja katika Kanisa na ushirikiano ili kuendelea kuitenda kazi ya Bwana.

Katika Mwendelezo wa ziara yake Askofu Dkt. Shoo ametembelea Usharika wa Bumbuli, Chuo cha Utabibu Bumbuli pamoja na Hospitali ya Bumbuli,Usharika wa Lutindi na Hospitali ya wagonjwa waakili (Lutindi Mental Hospitali),ambapo viongozi mbalimbali wa dini na Serikali wamehudhuria katika ziara hiyo huku akitazamiwa kuendelea na ziara yake hapo kesho katika Jimbo la Tambarare.




Awali Askofu Dkt. Fredrick Shoo alishiriki kwenye Ibada ya asubuhi iliyofanyika Makao Makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambapo alipata wasaa wa kuwasalimu wafanya kazi wa Ofisi kuu ya KKKT-DKMs.


Mapokezi Usharika wa Lutindi

