Idara ya Vijana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Jimbo la Pwani imefanya mkutano mkuu wa vijana ulikuwa na agenda ya uchaguzi wa viongozi wa vijana ngazi ya jimbo leo tarehe 27 Machi,2021 katika Usharika wa Kana Tanga.

Walio chaguliwa ni Bi.Monica Kitururu mwenyekiti kutoka Usharika wa Kana, Godchance Makamu  kutoka Usharika wa Makorora  .Jausia Mziray  Katibu kutoka Mission ya mto Pangani,Msuya ,Katibu Msaidizi kutoka Usharika wa Pangani na Anzamen Kileo  kutoka Usharika wa Kana amechaguliwa kuwa Mtunza hazina.

 WAJUMBE NI.

  1. Roda Yohana- Bethlehem
  2. Isaya Kifua Maramba

Viongozi mbali mbali wa vijana kutoka sharika za Jimbo la Pwani

Mwenyekiti wa vijana ngazi ya jimbo Bi.Monica Kitururu, akiwashukuru wajumbe mara baada ya uchaguzi.

 

 

 

Mkuu wa jimbo la Pwani (KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ) Mch. Thadeus Ketto  akisaini kitabu cha maombolezo na kutoa heshima za mwisho kwa HAYATI RAIS DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga .

 

Leo tarehe 10/01/2021 Askofu Mteule Mch Dkt Msafiri Joseph Mbilu mara baada ya Ibada katika Usharika wa Kana Jimbo la Pwani,amepata nafasi ya kufanya kikao na baadhi ya wazee wa Kanisa na Wazee maarufu wa Jimbo la Pwani. Kikao kilifanyika katika hostel ya Mbuyu Kenda Tanga lengo likiwa ni kupata maoni ya wazee hao juu ya namna bora ya kuiendeleza na kuiimarisha hostel ya Mbuyukenda.