ELCT North Eastern Diocese
Sehemu ya taarifa,picha za matukio na maelezo ziara ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu nchini Ujerumani.
- Details
Tarehe 21/09/2023 akiwa nchini Ujerumani Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alialikwa kwenye kiwanda cha kutengeneza makontena na stoo maalum zinazozuia moto, kiwanda hiki kinasimamiwa na kampuni ya DENIOS. Hapa Baba Askofu alikutana na baadhi ya marafiki walioonyesha moyo wa kujitolea kufadhili mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Makose kilichoko kwenye Usharika wa Mwangoi. Kutoka kulia ni Bw. Ernst-Ludwig Homann (anayesimamia mawasiliano kati ya Usaharika wa Mwangoi na Usharika rafiki wa Bergkirchen - Ujerumani), Bw. Helmut Dennig (Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya DENIOS) na Askofu Dkt. Mbilu. Mradi huu ambao utatekelezwa na kusimamiwa na Usharika rafiki wa Bergkirchen ni miongoni mwa miradi kadhaa ya maji iliyowekwa kwenye eneo la Usharika wa Mwangoi wa KKKT - Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.
- Hits: 320
Tuungane kwa pamoja kulikabili deni la Dayosisi, Dean Michael Kanju.
- Details
Msaidizi wa Askofu, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju amewashukuru Washarika wa Usharika wa Mgwashi na wanadayosisi kwa namna wanavyo endelea kujitoa kwa hali na mali kuchangia deni linaloikabili Dayosisi.
- Hits: 345
KATIKA PICHA, Mkutano Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani uliomaliziki hivi karibuni.
- Details
Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu akiwa na Cardinal Kurt Koch, ambaye alipata nafasi ya kufika kwenye Mkutano Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani (LWF), huyu ni kiongozi wa ngazi ya juu ndani ya Kanisa Katoliki. Cardinal Koch,ndiye anayehusika na maswala ya kuimarisha na kuendeleza Umoja wa Kikristo katika ofisi ya Papa, Vatican ( Prefect of the Vatican Dicastery for Promoting Christian Unity).
- Hits: 338
Ibada ya Kipaimara Usharika wa Kabuku, Jimbo Teule la Magharibi
- Details

- Hits: 413
Page 1 of 91