Leo tarehe 29/11/2020 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Handeni Jimbo la Tambarare Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMS) ambapo  vijana wapatao 9 walipata kipaimara na mmoja kati yao alibatizwa.Ibada hiyo iliongozwa na Mch.William Karata na Mch.Ismail Ngoda.Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti,Mashemasi,Kwaya,Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Handeni unao ongozwa na Mch Lewis F.Shemkala