KATIKA PICHA NI: Ziara ya Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,akiwa inchini Ujerumani. Katika ishara ya uhusiano thabiti na wa muda mrefu kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Kanisa la Westphalia la nchini Ujerumani, Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu alikuwa miongoni mwa viongozi wa Ibada kubwa ya kumsimika Mkuu mpya wa Kanisa la Ujerumani, Bishop Dkt. Adelheid Tuck-Schröder.
 
 
Ibada hii ya kihistoria ya kuingizwa kazini kwa kiongozi huyu wa juu wa Kanisa la Westphalia (Präses), ilifanyika Jumapili ya tarehe 15 Juni, 2025. Ushiriki wa Baba Askofu Dkt.Mbilu katika tukio hili muhimu unaashiria si tu heshima binafsi kwa Kiongozi huyo mpya wa Kanisa, bali pia unaimarisha uhusiano wa kindugu uliopo kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Kanisa la Westphalia.
 
 Kwa miaka mingi sasa KKKT-DKMs imekuwa na mahusiano mazuri na Kanisa la Westphalia yaliyojikita katika kubadilishana uzoefu wa kiroho, miradi ya maendeleo, na kusaidiana katika masuala mbalimbali ya kijamii na kiimani.
 
Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya kijamii
INSTAGRAM - / elctned
FACEBOOK ACCOUNT North Eastern Diocese
FACEBOOK PAGE - ELCT-North Eastern Diocese
YOUTUBE - / KKKT DKMS Online TV
KWA MAONI NA USHAURI:
Simu : +255 743 399 798