
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 21 Novemba, 2021 ameongoza Ibada ya Kipaimara katika Usharika wa Mgwashwi, Jimbo la Kusini.
Imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Mgwashwi ambapo jumla ya vijana wapatao 140 walibarikiwa na wawili kati yao walibatizwa.
Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu amewakumbusha vijana hao walio barikiwa kutokuondoka katika kweli ya neno la Mungu na kamwe wasiyumbishwe na mafundisho potofu ya neno la Mungu yaliyo kisiri katika nyakati hizi.

Katika salamu za Baba Askofu Dkt Msafiri Mbilu ameendelea kuwakumbusha wale wote waliopewa dhamana ya kutunza na kusimamia mali za Dayosisi kuhakikisha hakutokei upotevu wa mali au kitu chochote katika maeneo yao ikiwa ni katika Mashule,Hospitali, Majimbo,Sharika.
Aidha Baba Akofu Dkt. Mbilu ametoa ushauri kwa kwaya kuungana “Nimefika sehemu moja kwaya inawatu wanne nyingine watu nane nawasihi undeni kwaya zenye nguvu”, huku akitolea mfano kwaya kuu ya Kimara yenye waimbaji wapatao160, ameongeza kuwa kutakuwa na utaratibu maalumu wa kuangalia uimbaji wa kwaya pindi inapo hitaji kutoka nnje ya Dayosisi kwani zinaenda huku kuiwakilisha Dayosisi.

Uimbaji wakutumia nyimbo zilizwa rekodiwa na kutunzwa kwenye CD, DVD Pamoja na flash ni jambo linalo weza kupelekea kutokukuwa kwa uimbaji katika Dayosisi, Baba Askofu Mbilu ameziomba kwaya kujitahidi kuimba live huku wakitumia vyombo mbalimbali vya muziki.

Awali akitoa salamu za Ofisi kuu ya KKKT-DKMs, msaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju, amewashukuru washarika wa Usharika wa Mgwashi kwa namna wanavyo endelea kujitoa katika kazi mbalimbali za Usharika na Dayosisi kwa ujumla na kuwakumbusha kujiandaa na toleo maalumu la kuchangia kituo cha Redio Utume ambacho kipo katika mpango wa kupanua usikivu katika Mkoa wa Tanga.

Mch. Michael Kanju ameeleza kuwa utoaji wa taarifa ni dai la wana KKKT- DKMs hivyo uongozi utakuwa unatoa taarifa sahihi kila wakati,na kuhitimisha salamu zake kwa kuwahakikishia washarika wa Mgwashi kuwa uongozi upo imara na kamwe hawatawaangusha katika wajibu walio watuma.




