Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ametoa wito kwa watunzi wa nyimbo,mashairi, na sanaa mbalimbali kuendelea kutumia neno Kuu la Dayosisi linalo toka katika kitabu cha Zaburi ya 32:8 katika utunzi wao.

Wito huo ameutoa leo tarehe 01/01/2022 kwenye Ibada ya mwaka mpya iliyofanyika katika Usharika wa Vuga jimbo la Kusini.Baba Askofu Mbilu amesema kuwa bado ipo sababu ya kuendelea kufundishwa na kuoneshwa njia katika utumishi na hivyo neno kuu la mwaka jana litaendelea kutumika katika mwaka huu.

Kwa upande mwingine Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki imeona ni vema mwaka huu wa 2022 uwe mwaka wa wanawake kwani wanawake ni jeshi kubwa na imara hivyo wanao uwezo wa kuweka mipango mbalimbali na endelevu ili kuiinua na kuijenga Dayosisi.

Wito unaletwa kwa wanawake wote wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kuupokea mwaka huu kuanzia kwenye ngazi za Mitaa, Sharika, Majimbo hadi ngazi ya Dayosisi.ni matumaini ya uongozi wanawake wataweka mipango mbalimbali ili kuenzi mwaka huu.