Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju leo tarehe 21/05/2022 ameongoza Ibada iliyokuwa na tendo la kuwabariki vijana wa kipaimara katika Usharika wa Mshihwi Kanda ya Mto Umba Jimbo la Tambarare. Liturgia iliongozwa na Mkuu wa Jimbo hilo Mch. Frank Richard Mntangi.

Katika Risala ya vijana hao waliobarikiwa iliyosomwa mbele ya mzaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju vijana hao wameeleza kuwa wameona juhudi mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa Doyosisi katika kuirejesha Dayosisi katika hali nzuri, na hivyo vijana hao kuungana na uongozi katika juhudi hizo kwakutoa jumla ya Tsh.150,000. Jumla ya vijana 51 wamebarikiwa  wasichana 25 na wavulana 26.Ibada hii ya kipaimara nikiashiria cha kufunguliwa rasmi kwa kalenda ya matukio ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa mwaka 2022.