
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewakumbusha Wakristo kukemea matendo maovu ambayo yanajitokeza katika jamii hususani mmomonyoko wa maadili katika jamii ikiwemo suala la mapenzi ya jinsia moja.
Askofu Dkt. Mbilu ambaye ni Katibu wa (Chombo cha ki-ekumene cha Kikristo chenye kuleta maendeleo endelevu na kamilifu kwa ajili ya ufalme wa Mungu) CCT Mkoa wa Tanga ametoa wito huo leo tarehe 28/05/2023 wakati akitoa salamu zake katika ufunguzi wa tamasha la uimbaji la CCT lililofanyika Kanisa la Baptist Kisosora lililo jumuisha kwaya na washarika wa makanisa yaliyo chini ya Jumuiya ya Kikiristo Tanzania.
CCT ipo katika mkakati wa kuimarisha Umoja miongoni mwa Wanachama kwa kutumia CCT Day katika Mikoa. Mwaka huu 2023 kilele cha CCT Day kilifanyika Mkoani Kilimanjaro kikiongozwa na neno kutoka kitabu cha Yohana 13.35 “…..Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi”.


