
Hitimisho ya ziara ya ugeni kutoka Vyuo Vikuu vitano vilivyomuwakilisha Profesa Dkt. Ulrike Ludtke aliyewahi kuwa mhadhiri wa kilichokuwa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University (SEKOMU) mwaka 2008, ametembelea Dayosisi kwa makubaliano kati ya KKKT-DKMs na chama Cha kiinjili Cha Kimisioni (UEM: United Evangelical Mission) kwa lengo la kuanzisha kozi ya Lugha na mawasiliano (Speech and language therapy).

Profesa.Dkt. Ulrike alianzisha miradi mbalimbali ambayo iliunganisha kilichokuwa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University (SEKOMU) na kituo cha malezi ya watoto yatima (Irente Children's Home) lengo lilikua ni kukijengea uwezo kituo hicho kulea watoto kwa njia ya mafunzo maalum ambayo yalihusisha wanawake wa vijijini.

Wawakilishi hao ambao ni wataalam na wabobezi katika taaluma ya Lugha na mawasiliano (Speech and language therapy), wamefurahi jinsi KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kupitia uongozi wa Askofu Dkt Msafiri Mbilu unavyofanya kazi kwa uaminifu mkubwa, wameahidi kuendeleza ushirikiano huo na kuweka mpango mkakati wa kuboresha kituo hicho pamoja na kushirikiana na Taasisi ya Elimu ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI).


Wameweka alama ya ujio wao kwa kutoa zawadi katika vituo vinavyomilikiwa na KKKT-DKMS ambavyo ni Irente Children's Home, Irente Rainbow School na Irente School for the Blind.

