Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt. Msafiri Joseph Mbilu pamoja na ujumbe kutoka Bethel Ujerumani leo wameanza ziara ya kutembelea vituo vinavyomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kwa lengo la kushirikiana katika kuviendeleza kwa pamoja vituo hivyo.

Kwa siku ya leo tarehe 26/06/2023 vituo vilivyo tembelewa ni Taasisi ya Kolowa Technical Training Institute (KOTETI), Irente Children's Home, Irente School for the Blind pamoja na Rainbow School ambapo katika vituo hivyo vyote ugeni huu umepata maelezo ya namna vituo hivyo vinavyo endeshwa kutoka kwa wakuu wa vituo hivyo

Askofu Dkt. Mbilu akiwa katika kituo cha Irente Children's Home hakusita kuwashukuru wale wote wanaofika katika kituo hicho kwa namna wanavyo jitoa kwa hali na mali kukisaidia kituo hicho ambacho kimekuwa msaada mkubwa katika kuwalea Watoto wanaokutana na changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Mdiakonia Kathrin Steinkampm amefurahishwa kwa kiasi kikubwa kwa kuona upana wa kazi kubwa inayofanyika katika kituo cha Irente Children's Home kwa namna Watoto wanavyo tunzwa vizuri na uwepo wa Watoto kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo Bukoba.

Ujumbe huu unaongozwa na Mkuu wa Taasisi ya Diakonia Bethel nchini Ujerumani Mdiakonia Kathrin Steinkamp ambaye ameanza kazi rasmi mwezi Agosti 2022 akichukua nafasi ya Regine Buschmann aliyestaafu.

Askofu Dkt. Mbilu akiweka sahihi kwenye  kitabu cha wageni (Irente Children's Home) kushoto ni Mdiakonia Kathrin Steinkamp.