MATUKIO KATIKA PICHA . Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,Tarehe: 26/10/2023, akiwa katika ziara ya kikazi katika Jimbo la Magharibi, Usharika wa Gombero, ambapo kumefanyika Ibada zilizoambatana na matendo mbalimbali.
Baba Askofu akiwa katika Mtaa wa Kileguru alifungua Nyumba ya mtumishi, baada ya hapo alielekea katika Mtaa wa Gitu Juu ambapo katika Mtaa huo aliweka Jiwe la Msingi la Kanisa na kufungua Kanisa hilo. Katika Mtaa wa Kibirashi Baba Askofu aliweka jiwe la Msingi la Nyumba ya mtumishi na kufungua nyumba hiyo. Baada ya hapo aliweka jiwe la Msingi la Kanisa katika Mtaa huo huo wa Galilaya Kibirashi.Katika Ibada hizi zilizofanyika katika Mitaa hii ya Usharika wa Gombero,kiasi cha Tsh. 683,400 kilikusanywa kwaajili ya kuchangia ulipaji wa deni la Dayosisi.