Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu yupo katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani ambapo ameambatana na Dean Mteule Frank Mtangi pia wamepata wasaa wa kutembelea Jimbo la Staaken kwenye Jiji la Berlin.
Askofu Dkt Mbilu aliongoza Ibada ya Jumapili ya tarehe 27/04/2025, ziara hii ya kikazi imekua na vikao mbalimbali vya kuimarisha urafiki na umoja katika kuleta maendeleo chanya ya KKKT-DKMs. Katika kikao hiki Jimbo la Staaken limeamua kuweka nguvu kubwa katika kusaidia Kituo cha Watoto yatima Irente.
 
Askofu Dkt. Mbilu na Dean Mteule Mntangi wapo katika Mji wa Hannover kushiriki Sikukuu ya Kanisa inayoitwa kwa Kijerumani Kirchentag. Sikukuu hii ya Kanisa la Kiinjili Ujerumani inahudhuriwa na Wakristo wengi sana,na watu 100,000 walishiriki katika Ibada ya Ufunguzi. Sikukuu hii ya Kanisa ilianza tangia tarehe 30/04/2025 hadi tarehe 4/5/2025 Hannover Ujerumani.
Ibada ilipambwa na kikundi cha Tarumbeta cha wapigaji wapatao 3000 na Waimbaji 1200 na Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ambapo mara baada ya Ibada hiyo Askofu Dkt. Mbilu alipata nafasi ya kufanya mazungumzo na Rais wa Ujerumani kuhusu Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.