Msaidizi wa Askofu kutoka KKKT Dayosisi ya Karagwe, Mch Yared A. Wakami ameipongeza KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  hususani wafanya kazi wa vituo vya Irente Rainbow School,Irente School for the Blind,Irente Farm pamoja na kituo cha Irente Children’s Home kwa namna wanavyo tumika kwa uaminifa katika kuvitunza vituo hivyo.

 

Mch Yared A. Wakami  ametoa pongezi hizo  leo tarehe 15/06/2021 alipotembelea vituo hivyo vinavyo milikiwa na KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambapo  imekuwa ni mwendelezo wa ziara yake KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Katika ziara hii Mch Yared Apolo Wakami aliambatana na mwenyeji wake, msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Michael M. Kanju,Awali Mch Yared A. Wakami  alipata nafasi ya kuongoza Sala ya Asubuhi pamoja na kutembelea Makao Makuu ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

 UEM: United Evangelical Mission ni chama Cha kiinjili Cha kimisioni kilichoanzishwa miaka 25 iliyopita na wamisionari kutoka Ijerumani wa Rhenish na Betheli ambao walifika Africa, na Asia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za Dini. Katika Africa walifika katika nchi 7 amabazo ni Tanzania, DR Congo, Africa ya Kusini, Botswana, Cameroon, Namibia na Namibia na Rwanda kukiwa na madhehemu 15. Katika Tanzania inawakilishwa na Makanisa 4 ya KKKT ambayo ni KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na KKKT Dayosisi ya Karagwe.

Aidha Chama hiki kinashughulika katika nguzo tano ambazo ni Uhusiano/ Undugu, Diakonia, Uinjilishaji, Utetezi pamoja na maendeleo. KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ni miongoni mwa Dayosisi muhimu sana na kitovu cha chama hiki cha kiinjili cha kimisioni.