
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu,amewapongeza washarika wa Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Saruji kwa moyo wakujitoa katika kumtumikia Mungu.

Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 29/11/2021 kwenye Ibada ya uwekwaji wa jiwe la msingi na ufunguzi wa darasa la Watoto wa shule ya Jumapili, mahali ambapo Watoto hao wataabudia.

Baba Askofu Dkt. Mbilu kama ishara ya kutambua umuhimu wa Watoto wa Shule ya Jumapili kujengewa sehemu nzuri za kuabudia ametoa kiasi cha Tsh laki moja 100,000 kuunga mkono juhudi za uongozi wa Usharika wa Pongwe, Mtaa wa Saruji pamoja na wazazi.


Baba Askofu Mbilu hapo kesho ataweka Jiwe la Msingi la Shule ya Watoto wa Jumapili katika Usharika wa Pongwe Mtaa wa Saruji,Kuweka jiwe la msingi la Kanisa katika Usharika wa Pongwe mtaa wa Machemba pamoja na kufungua Kanisa katika Usharika wa Pongwe mtaa wa Kilapula.







